UNHCR: Wahajiri 220 waaga dunia katika pwani ya Libya
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i46176-unhcr_wahajiri_220_waaga_dunia_katika_pwani_ya_libya
Watu walionusurika kifo wameeleza kuwa wahajiri wenzao wasiopungua 220 wameaga dunia katika pwani ya Libya katika siku kadhaa za karibuni wakijaribu kuelekea Ulaya.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Jun 22, 2018 08:04 UTC
  • UNHCR: Wahajiri 220 waaga dunia katika pwani ya Libya

Watu walionusurika kifo wameeleza kuwa wahajiri wenzao wasiopungua 220 wameaga dunia katika pwani ya Libya katika siku kadhaa za karibuni wakijaribu kuelekea Ulaya.

Kiwango hicho cha wajahiri walioga dunia huko Libya kinaifanya idadi ya vifo vya wahajiri waliokuwa wakijaribu kuelekea barani Ulaya mwaka huu kufikia zaidi ya 1000.

Hayo yametangazwa na Kamisheni Kuu ya Wakimbizi ya Umoja wa Mataifa. Kikosi cha ulinzi katika pwani ya Libya siku mbili zilizopita kiliwaokoa na kuwapakia katika boti za plastiki wahajiri wasiopungua 762 waliokuwa katika harakati za kuelekea Ulaya.  

Nchi ya Libya inayopatikana kaskazini mwa Afrika inatumiwa kama lango kuu la kutorosha wahajiri wanaotaka kufika Ulaya wanaokimbia vita na umaskini katika nchi zao; ingawa wimbi la uvukaji wahajiri limepungua sana tangu mwezi Julai mwaka uliopita kutokana na ulinzi mkali katika pwani ya nchi hiyo.