Jun 24, 2018 12:50 UTC
  • Afisa wa serikali na Wafaransa 4 watiwa nguvuni kwa ufisadi Burundi

Serikali ya Burundi imemtia nguvuni afisa mmoja wa ngazi ya juu wa nchi hiyo na raia wanne wa Ufaransa kwa tuhuma za kufanya utapeli.

Wizara ya Usalama wa Umma ya Burundi imetangaza kuwa, watuhumiwa hao watano wanahusishwa na uhalifu wa kughushi, ubadhirifu na kufanya utapeli katika sekta ya mawasiliano nchini humo. 

Taarifa ya wizara hiyo imesema wawili kati ya raia hao wanne wa Ufaransa wamekamatwa katika uwanja wa ndege wa Bujumbura wakiwa mbioni kutoroka nchi. 

Afisa wa serikali aliyetiwa nguvuni nchini Burundi alikuwa mshauri wa rais wa wa jamhuri na mkurugenzi wa mashirika kadhaa ya mawasiliano nchini humo.  

Tags