Watu 75 wauawa na kujeruhiwa katika mapigano ya kikabila Sudan Kusini
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i47438-watu_75_wauawa_na_kujeruhiwa_katika_mapigano_ya_kikabila_sudan_kusini
Maafisa wa serikali ya Sudan Kusini wametangaza kuwa watu 23 wameuliwa na wengine 52 wamejeruhiwa katika mapigano ya kikabila yaliyotokea magharibi mwa nchi hiyo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Aug 14, 2018 10:31 UTC
  • Watu 75 wauawa na kujeruhiwa katika mapigano ya kikabila Sudan Kusini

Maafisa wa serikali ya Sudan Kusini wametangaza kuwa watu 23 wameuliwa na wengine 52 wamejeruhiwa katika mapigano ya kikabila yaliyotokea magharibi mwa nchi hiyo.

Idara kuu ya habari ya jimbo la Tonj imeripoti kuwa mapigano hayo yametokea katika kipindi cha siku tatu zilizopita baada ya wafugaji wanne wa kabila wa Dinka kuuliwa wakati walipovamiwa na watu waliotaka kuiba mifugo yao.

Kufuatia hujuma hiyo, watu wa kabila la Dinka waliamua kulipiza kisasi kwa watu wa kabila jirani waliowadhani kuwa ndio waliohusika na mauaji ya wenzao, ambapo katika ulipizaji kisasi huo watu 75 waliuawa na kujeruhiwa.

Mfugaji wa kabila la Dinka

Machafuko na mapigano yanayotokana na mifugo ni changamoto kubwa na ya miongo kadhaa kwa serikali ya Sudan Kusini ambapo maelfu ya watu wameshauawa hadi sasa katika mapigano ya aina hiyo.../