Sep 23, 2018 07:58 UTC
  • Katumbi: Matokeo ya uchaguzi wa Kongo DR kuyumbisha uthabiti Afrika

Moise Katumbi, mwanasiasa wa upinzani wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ambaye kwa sasa yuko uhamishoni nchini Ubelgiji ametadharisha kuwa, matokeo ya uchaguzi wa rais utakaofanyika nchini humo mwishoni mwa mwaka huenda yakavuruga amani na uthabiti sio tu katika nchi hiyo bali kote barani Afrika.

Katika mahojiano na shirika la habari la City Press, Katumbi ambaye amewahi kuwa Gavana wa Gatanga ameitaka Jumuiya ya Ustawi ya Nchi za Kusini mwa Afrika SADC kutosubiri mambo yavurugike nchini humo na kusisitiza kwamba huu ndio wakati mwafaka wa kushughulikia kadhia ya kisiasa ya nchi hiyo.

Mwezi uliopita, Katumbi alidai kuwa, ndege yake binafsi ilinyimwa kibali cha kutua mjini Lubumbashi, kutokana na kile vyombo vya dola vinadai kuwa ni mashtaka yanayoendelea kumkabili mwansiasa huyo.

Ofisi ya mashtaka ilitangaza kwamba Moise Katumbi hatoruhiwa kuwania urais na atakamatwa akiwasili nchini DRC kwa kosa la kuhatarisha usalama wa taifa.

Rais Joseph Kabila

Moise Katumbi anakabiliwa na mashtaka ya kuajiri askari mamluki kwa lengo la kuangusha utawala wa Rais Joseph Kabila, ambaye amekuwa madarakani kwa kipindi cha miaka 17.

Uchaguzi wa rais DRC unatazamiwa kufanyika Disemba 23 mwaka huu.

Tags