Sep 30, 2018 14:25 UTC
  • Serikali ya umoja wa kitaifa Libya yaunga mkono mchakato wa uchaguzi

Waziri Mkuu wa serikali ya umoja wa kitaifa ya Libya amekutaja kufanyika chaguzi za bunge na rais nchini humo kuwa njia bora zaidi kwa ajili ya kurejesha amani nchini humo.

Fayez al Sarraj Waziri Mkuu wa serikali ya umoja wa kitaifa ya Libya amekutana na kufanya mazungumzo na Emad al Sayah Mkuu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya nchi hiyo na kubainisha hamu yake ya kuiunga mkono tume hiyo ili kutekeleza majukumu yake. Al Sarraj ameongeza kuwa kufanyika chaguzi hizo zilizotajwa ni njia bora zaidi itakayosaidia kuhitimisha kipindi cha mpito na kurejesha amani huko Libya. 

Pande mbili hizo aidha zimechunguza mchakato wa uchaguzi na namna Tume ya Taifa ya Uchaguzi ilivyojiandaa kuendesha uchaguzi yakiwemo maandalizi ya masuala ya kiufundi. Makundi ya kisiasa ya Libya mwezi Mei mwaka huu yaliitisha kikao mjini Paris Ufaransa na kutoa taarifa waliyoipa jina la "Tamko la Paris". Makundi hayo yalikubaliana pia kuhusu kufanyika chaguzi hizo mbili  tarehe 10 Disemba mwaka huu.  

Makundi ya kisiasa ya Libya katika mkutano wa Paris 

 

Tags