Somalia yamfukuza mjumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i50573-somalia_yamfukuza_mjumbe_wa_umoja_wa_mataifa_nchini_humo
Wizara ya Mambo ya Nje ya Somalia imesema kuwa Nicholas Haysom, mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa hatakiwi nchini humo na imemtaka aondoke haraka Somalia.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jan 01, 2019 23:40 UTC
  • Somalia yamfukuza mjumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo

Wizara ya Mambo ya Nje ya Somalia imesema kuwa Nicholas Haysom, mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa hatakiwi nchini humo na imemtaka aondoke haraka Somalia.

Shirika la habari la IRNA limeinukuu wizara hiyo ya mambo ya nje ya Somalia ikisema kuwa, uamuzi huo umechukuliwa kutokana na miamala mibaya ya Haysom na kuingilia kwake waziwazi mambo ya ndani ya Somalia.

Wizara hiyo imeongeza kuwa, tayari Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, António Guterres ameshapewa taarifa rasmi kuhusu uamuzi huo.

Mukhtar Robow

 

Itakumbukwa kuwa, juzi Jumatatu, Haysom aliwataka viongozi wa Somalia watoe maelezo kuhusu kutiwa mbaroni Mukhtar Robow, mmoja wa viongozi wa zamani wa genge la kigaidi la al Shabab ambaye pia aliwahi kuwa mgombea katika uchaguzi wa nchi hiyo, pamoja na wafuasi wake 15 waliowekwa nguvuni wakati wa maandamano ya tarehe 13 Disemba 2018 mjini Baidoa.

Mwezi Septemba 2018, Nicholas Haysom aliteuliwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres kuwa mjumbe maalumu wa umoja huo katika masuala ya Somalia.