Magaidi 77 wa al-Shabaab wauawa kusini mwa Somalia
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i50997-magaidi_77_wa_al_shabaab_wauawa_kusini_mwa_somalia
Jeshi la Somalia limefanikiwa kuangamiza wanachama 77 wa kundi la kigaidi na kitakfiri la al-Shabaab kusini mwa nchi hiyo ya Pemba ya Afrika.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jan 20, 2019 04:29 UTC
  • Magaidi 77 wa al-Shabaab wauawa kusini mwa Somalia

Jeshi la Somalia limefanikiwa kuangamiza wanachama 77 wa kundi la kigaidi na kitakfiri la al-Shabaab kusini mwa nchi hiyo ya Pemba ya Afrika.

Jenerali Aden Goojar, kamanda mkuu wa jeshi katika jimbo la Jubaland amesema wanajeshi wa Somalia wakishirikiana na askari wa Marekani wamefanikiwa kuzima hujuma ya matakfiri hao waliojaribu kuvamia kambi ya jeshi jana Jumamosi katika eneoa la Sanguuni, nje kidogo ya mji bandari wa Kismayu, kusini mwa Somalia.

Amesema gari la magaidi hao lililokuwa limesheheni mabomu liliripuliwa kabla ya kufika katika kambi hiyo. 

Wakati huohuo, Kamandi Kuu ya Jeshi la Marekani barani Afrika (Africom) imeripoti kuwa, jeshi la US limefanya mashambulizi ya anga dhidi ya ngome za al-Shabaab na kufanikiwa kuua wanachama 52 wa genge hilo.

Wanajeshi wa Somalia

Mohamed Abdikarin, afisa wa ngazi za juu wa jeshi la Somalia ameliambia shirika la habari la AFP kuwa, wanajeshi wa Somalia, Jubbaland na Marekani waliwakabili vikali wanamgambo wa al-Shabaab ambao jana walivamia kambi ya jeshi katika mji wa Bulogagdud huku wakiwa wamejizatiti kwa silaha na mada za miripuko.

Ameongeza kuwa, askari sita wa Somalia wameuawa pia katika makabiliano hayo ya genge hilo la ukufurishaji, ambalo siku chache zilizopita lilitangaza kuhusika na shambulizi la kigaidi dhidi ya hoteli moja ya kifahari katika mji mkuu wa Kenya, Nairobi, ambapo watu 21 waliuawa.