Apr 18, 2016 04:14 UTC
  • Angola; nchi ya kwanza kwa kuzalisha mafuta barani Afrika

Angola hivi sasa imekuwa nchi ya kwanza inayozalisha mafuta kwa wingi barani Afrika.

Jumuiya ya Nchi Zinazozalisha Mafuta kwa Wingi Duniani (Opec) imetangaza kuwa Angola mwezi Machi mwaka huu ilizalisha mapipa ya mafuta milioni moja, laki saba na elfu 82 kwa siku na hivyo kuwa nchi ya kwanza inayozalisha mafuta mengi barani Afrika ikifuatiwa na Nigeria.

Jumuiya ya Opec imeeleza kuwa kiwango hicho kinaonyesha kuongezeka uzalishaji mafuta wa Angola kwa mapipa elfu 15 kwa siku ikilinganishwa na mwezi Februari. Mwezi Machi mwaka huu, Nigeria kwa siku ilikuwa ikizalisha mapipa ya mafuta milioni moja, laki sita na elfu sabini na mbili. Ripoti ya Opec imeongeza kuwa Angola pamoja na Iran na Iraq zimekuwa na ongezeko kubwa la uzalishaji wa mafuta. Kuhusiana na suala hilo pia Angola imetangaza kuwa nchi hiyo itaweza kuzalisha mapipa ya mafuta milioni mbili hadi miaka mitatu ijayo kufuatia kugunduliwa akiba kubwa ya mafuta nchini humo.

Tags