Pars Today
Balozi mpya wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Angola na rais wa nchi hiyo wamelaani vitendo vya jinai vya utawala wa Kizayuni wa Israel katika Ukanda wa Gaza na Lebanon.
Angola imesema itatuma kikosi cha wanajeshi wake mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, siku chache baada ya makubaliano ya kusitisha vita baina ya pande hasimu nchini humo kugonga mwamba.
Sergei Lavrov Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Russia amezituhumu nchi za Magharibi kwa kuzishinikiza nchii zinazoendelea duniani ilikuegemea na kuiunga mkono Ukraine.
Mahakama ya Juu ya Angola imeamuru kuzuiliwa "kitahadhari" mali zenye thamani ya takriban dola bilioni moja zinazomilikiwa na Isabel dos Santos, binti wa rais wa zamani wa nchi hiyo José Eduardo dos Santos.
Mahakama ya Katiba ya Angola imetupilia mbali kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi wa rais wa Agosti 24, yaliyompa ushindi mgombea wa chama tawala cha MPLA, Rais Joao Lourenco.
Matokeo ya awali katika uchaguzi mkuu uliofanyika nchini Angola hapo jana yanaonesha kuwa chama tawala cha MPLA kinaongoza.
Wananchi wa Angola waliotimiza masharti ya kupiga kura leo wanashiriki katika uchaguzi kwa ajili ya kumchagua rais mpya wa nchi hiyo.
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, DRC na Rwanda zimekubaliana kutekeleza "mchakato wa kupunguza mvutano" baina yao kufuatia mazungumzo ya siku moja yaliyofanywa na marais wa nchi hizo mbili kwa upatanishi wa rais wa Angola.
Zaidi ya nusu ya madaktari wote nchini Angola wanaendelea na mgomo wao wa nchi nzima wakishinikiza kulipwa mishahara yao na kuboreshewa mazingira ya kazi huku janga la corona likiendelea kuutatiza mfumo dhaifu wa huduma za afya wa nchi hiyo.
Watoto 144 wamepoteza maisha kutokana na utapiamlo katika kipindi cha miezi sita ya kwanza ya mwaka huu katika mkoa wa Bié katikati mwa Angola.