Jan 26, 2023 09:09 UTC
  • Lavrov ziarani Angola katika juhudi za kuungwa mkono kimataifa Moscow

Sergei Lavrov Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Russia amezituhumu nchi za Magharibi kwa kuzishinikiza nchii zinazoendelea duniani ilikuegemea na kuiunga mkono Ukraine.

Lavrov amebainisha haya akiwa ziarani huko Luanda mji mkuu wa Angola katika marha nyingine ya ziara yake barani Afrika ilikuvutia uungaji mkono wa kimataifa kwa Moscow.Vita vinavyoendelea Ukraine viligubika ajenda ya mazungumzo kati ya Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Russia na viongozi wa ngazi ya juu wa serikali ya Angola; ambao wamemtaka Lavrov ifanyike tathmini kuhusu hali ya mambo katika medani ya vita huko Ukraine. 

Mkuu huyo wa chombo cha diplomasia wa Russia amezinyoshea kidole cha lawama nchi za Magharibi na kuzituhumu kwa kuiburuta Ukraine katika vita mseto na vya niaba dhidi ya Russia. Itakumbukwa kuwa Angola ilijizuia kupinga kura Umoja wa Mataifa kulaani uvamizi wa Russia dhidi ya Ukraine, Bali mwezi Oktoba mwaka jana Luanda ilipiga kura ikiunga mkono azimio la kulaani hatua ya Russia ya kudhibiti baadhi ya maeneo ya Ukraine. 

Aidha mapema mwezi huu, Rais João Lourenço wa Angola aliitolea wito Russia kusitisha vita bila ya masharti yoyote. Russia na Angola zinajitayarisha kwa ajili ya mkutano wa pili wa pande mbili kuwahi kufanyika katika historia ya nchi mbili hizo. Mkutano huo umepangwa kufanyika mwezi Aprili mwaka huu huko Luanda.  

Rais Joao Laurenco wa Angola 

Jumatatu wiki hii pia Sergei Lavrov  alikutana na kuzungumza mjini Pretoria Afrika Kusini na Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo bi Naledi Pandor. Maafisa wa serikali ya Afrika Kusini waliitaja ziara hiyo ya Lavrov nchini humo kuwa ni ya kawaida lakini ambayo haijapewa uzito na baadhi ya vyama vya siasa na jamii ndogo ya raia wa Ukraine waishio nchini Afrika Kusini. 

Tags