Musa Ibrahim: Libya imeharibiwa kwa lengo la kupora tena utajiri wa Afrika
(last modified Tue, 08 Oct 2019 04:38:08 GMT )
Oct 08, 2019 04:38 UTC
  • Musa Ibrahim: Libya imeharibiwa kwa lengo la kupora tena utajiri wa Afrika

Msemaji wa zamani wa utawala wa Libya amesema kuwa Muungano wa Kijeshi wa Nchi za Magharibi (Nato) umevamia na kuibomoa Libya lengo lake likiwa ni kuendelea kupora utajiri wa Afrika.

Musa Ibrahim mmoja wa waliokuwa wasemaji wa Muammar Gaddafi dikteta wa Libya aliyepinduliwa madarakani amesema kuwa muungano wa Nato huku ukiongozwa na Marekani uliishambulia Libya mwaka 2011 na hivyo kuondoa vizuizi vilivyokuwepo ili kuweza kupora utajiri wa Afrika. Libya ilitumbukia katika hali ya mchafukoge baada ya kupinduliwa utawala wa Gaddafi mwezi Oktoba mwaka 2011 na kutokana na uingiliaji kijeshi wa muungano wa Nato na muitifaki wake Marekani.

Pamoja na kuwa serikali ya umoja wa kitaifa ya Libya yenye makao yake katika mji mkuu Tripoli inaungwa mkono na Umoja wa Mataifa lakini Marekani na Saudi Arabia kwa upande wao zinawaunga mkono wanamgambo wanaoongozwa na jenerali muasi Khalifa Haftar kwa jina la jeshi la kitaifa la Libya.