Benki ya Dunia: Ukuaji wa uchumi wa Tanzania kupungua sana
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i61509-benki_ya_dunia_ukuaji_wa_uchumi_wa_tanzania_kupungua_sana
Benki ya Dunia imekadiria kuwa kutokana na mlipuko wa COVID-19, ukuaji wa uchumi wa Tanzania mwaka huu utapungua sana na kufikia asilimia 2.5 kutoka asilimia 6.9 kama ilivyokadiriwa na serikali mwaka 2019.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jun 10, 2020 00:07 UTC
  • Benki ya Dunia: Ukuaji wa uchumi wa Tanzania kupungua sana

Benki ya Dunia imekadiria kuwa kutokana na mlipuko wa COVID-19, ukuaji wa uchumi wa Tanzania mwaka huu utapungua sana na kufikia asilimia 2.5 kutoka asilimia 6.9 kama ilivyokadiriwa na serikali mwaka 2019.

Benki ya Dunia imesema uchumi wa Tanzania utaathiriwa na janga la COVID-19 na msukosuko wa uchumi wa dunia.

Ripoti hiyo iliyotolewa na Benki ya Dunia imesema kuwa serikali ya Tanzania imechukua hatua, na inatarajiwa kuendelea kuchukua hatua za ziada za kiafya na kiuchumi, ili kupunguza athari hasi.

Lakini ripoti hiyo, ambayo ni ya 14 ya Benki ya Dunia kuhusu uchumi wa Tanzania, pia imeonya kuwa, kama hatua za ziada zitacheleweshwa au hazitafanya kazi, na kama mazingira ya nje hayataboreka mwaka huu, ukuaji wa uchumi wa Tanzania huenda utapungua zaidi.

Rais Dkt. John Pombe Magufuli wa Tanzania

Tathmini ya ripoti hiyo ya Benki ya Dunia inaonyesha kuwa janga la COVID-19 limevuruga maisha ya wananchi wa kawaida ambapo imetabiriwa kuwa  Watazania nusu milioni wataingia katika kundi la watu wanaoishi chini ya mstari wa umasikini. Watakaoathirika zaidi ni watoto wanaoishi mijini ambao wamejiajiri na wenye biashara ndogo ndogo.