Afrika Kusini: Tupo tayari kuisaidia Msumbiji iliyokumbwa na mashambulizi ya magaidi
(last modified Thu, 03 Sep 2020 11:12:39 GMT )
Sep 03, 2020 11:12 UTC
  • Afrika Kusini: Tupo tayari kuisaidia Msumbiji iliyokumbwa na mashambulizi ya magaidi

Waziri wa Mambo ya Nje wa Afrika Kusini amesemam kuwa nchi hiyo iko tayari kuisaidia Msumbiji iliyoathiriwa na mashambulizi ya wanamgambo wenye mfungamano na kundi la Daesh yaani ISIS.

Afrika Kusini imesema kuwa iko tayari kumsaidia jirani yake huyo kwa msaada wa kiitelijinsia au kijeshi iwapo itaombwa kufanya hivyo.  

Wanamgambo wenye mfungamano na kundi la kigaidi la Daesh mwaka huu wamefanya mashambulizi kadhaa huko Msumbiji. Naledi Pandor Waziri wa Mambo ya Nje ya Afrika Kusini ameiambia kamati ya bunge la nchi hiyo kwamba, Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC)  imeitaka Msumbiji iwasilishe ramani ya njia kuhusu misaada itakayohitajia.  

Mamluki wa kundi la Daesh washadidisha mashambulizi Msumbiji  

Jimbo la Cabo Delgado huko kaskazini mwa Msumbiji lilianza kushuhudiwa mashambulizi ya wanamgambo wenye mfungamano na kundi la Daesh mwaka 2017. Mashambulizi hayo yaliongezeka sana mwaka huu na kusababisha kudhibitiwa miji muhimu kwa muda kadhaa sambamba na kushambuliwa maeneo ya kijeshi na yale ya kistratejia. 

Waziri wa Mambo ya Nje wa Afrika Kusini ameongeza kuwa, Msumbiji imekuwa ikishirikiana vizuri na wanachama wengine wa Sadc na kwa msingi huo tunatafuta njia kuona ni kwa jinsi gani tunaweza kuisaidia katika uwanja huo.