-
Kadhaa wauawa katika shambulizi la kigaidi kaskazini mwa Msumbiji
Apr 10, 2025 02:54Watu wasiopungua watano wameuawa huku wengine kadhaa wakijeruhiwa vibaya katika shambulio la kigaidi katika jimbo la Cabo Delgado, kaskazini mwa Msumbiji.
-
Bunge la Msumbiji lapasisha sheria kuhusu mazungumzo ya kitaifa ili kurejesha amani
Apr 03, 2025 11:34Bunge la Msumbiji kwa kauli moja limepaisha sheria ili kurejesha amani katika nchi hiyo ya kusini mwa Afrika kufuatia miezi kadhaa ya maandamano makubwa ya ghasia ya wananchi ya kupinga matokeo ya uchaguzi wa rais uliofanyika Oktoba 9. Watu takriban 360 walipoteza maisha katika maandamano hayo ya ghasia.
-
SADC yataka kuhitimisha uhasama haraka iwezekanavyo nchini Msumbiji
Jan 01, 2025 03:40Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) jana Jumanne ilitoa wito wa kuhitimishwa mara moja uhasama na mivutano inayoendelea huko Msumbiji ambapo watu 278 wameuawa tangu chama kikuu cha upinzani kipinge matokeo ya uchaguzi wa Rais wa mwezi Oktoba.
-
Kimbunga Chido kinazidi kuteketeza roho za watu huko Msumbiji; Watu 94 wameaga dunia
Dec 23, 2024 14:15Taasisi ya Taifa ya Kushughulikia Majanga ya Kimaumbile ya Msumbiji (INGD) imetangaza kuwa kimbunga Chido hadi sasa kimeuwa watu 94 nchini humo tangu kilipoiathiri nchi hiyo wiki iliyopita.
-
Kimbunga Chido chaikumba Msumbiji; UN yatenga dola milioni 4 kwa ajili ya nchi hiyo
Dec 18, 2024 12:56Umoja wa Mataifa umetenga dola za kimarekani milioni 4 kuisaidia Msumbiji kukabiliana na athari mbaya za kimbunga cha kitropiki, Chido kilichopiga maeneo ya pwani nchini humo siku ya Jumapili.
-
Watu 5 wapoteza maisha katika maandamano ya ghasia nchini Msumbiji
Dec 06, 2024 12:25Polisi ya Msumbiji imeripoti kuwa watu wasiopungua watano wamepoteza maisha na wengine watatu wamejeruhiwa vibaya katika maandamano ya ghasia katika miji ya Maputo, Nampula na Zambezia.
-
Polisi Msumbiji yakamata kilo 573 za kokeini katika meli ya India
Nov 13, 2024 02:19Polisi ya Msumbiji imekamata kilo 573 sawa na (pauni 1,263) za dawa za kulevya aina ya kokeini katika meli ya India. Haya yameelezwa na Idara ya Taifa ya Upelelezi ya nchi hiyo.
-
Jeshi latumwa mitaani kuzima ghasia za baada ya uchaguzi Msumbiji
Nov 09, 2024 03:19Msumbiji imetuma wanajeshi mitaani kusaidia kudumisha utulivu kufuatia wiki kadhaa za maandamano ya ghasia dhidi ya chama tawala ambacho kinatuhumiwa kwa udanganyifu katika uchaguzi wa mwezi uliopita.
-
Mkuu wa Umoja wa Afrika alaani ghasia za baada ya uchaguzi nchini Msumbiji
Oct 21, 2024 11:47Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika Moussa Faki Mahamat leo Jumatatu amelaani mauaji ya viongozi wawili wa upinzani nchini Msumbiji na kutaka uchunguzi ufanyike ili wahusika wafikishwe mbele ya sheria.
-
Wananchi wa Msumbiji wapiga kura kumchagua rais na wabunge
Oct 09, 2024 10:59Raia wa Msumbiji wasiopungua milioni 17 waliojiandikisha kupiga kura mapema leo walielekea katika vituo vya kura kwa lengo la kumchagua rais mpya, wawakilishi wa bunge na magavana wa majimbo ya nchi hiyo katika uchaguzi unaotazamiwa kwa kiasi kikubwa kukibakisha madarakani chama tawala cha FRELIMO ambacho kimekuwa madarakani kwa miaka 49 sasa.