Bunge la Msumbiji lapasisha sheria kuhusu mazungumzo ya kitaifa ili kurejesha amani
Bunge la Msumbiji kwa kauli moja limepaisha sheria ili kurejesha amani katika nchi hiyo ya kusini mwa Afrika kufuatia miezi kadhaa ya maandamano makubwa ya ghasia ya wananchi ya kupinga matokeo ya uchaguzi wa rais uliofanyika Oktoba 9. Watu takriban 360 walipoteza maisha katika maandamano hayo ya ghasia.
Bunge lal Msimbiji lenye wabunge 250 limepasisha sheria kwa ajili ya kuandaa Mazungumzo ya Kitaifa Jumuishi, sheria ambayo inalenga kurekebisha katiba ya nchi na mamlaka ya rais, na kutoa msamaha kwa wale waliopatikana na hatia ya kuhusika na ghasia za machafuko baada ya uchaguzi.
Sheria hiyo inayoelezwa kuwa ni ya "kihistoria" inayojumuisha pande zote mbili yaani mahasimu wa kisiasa katika Bunge la Taifa la Msumbiji, inatokana na makubaliano yalitofikiwa Machi 5 na kusainiwa na Rais Daniel Chapo na vyama vyote vya kisiasa nchini humo.
Eduardo Mulembwe Waziri katika ofisi ya Rais anayehusika na masuala ya bunge, serikali za mitaa na majimbo amesema muda mfupi baada ya kupasishwa sheria hiyo kwamba itaruhusu raia kusafiri kwa amani na usalama, katika barabara na njia zote."
" Sheria hii inafungua zamam mpya za amani, na itaruhusu wananchi wote kufanya kazi kwa bidii na kusafirisha mali zao katika pembe zote za nchi; imma iwe ni kibiashara au kwa ajili ya mahitaji ya familia bila ya kuofia chochote", amesema Eduardo Mulembwe.
Wakati huo huo, Felix Silvia kiongozi wa chama tawala cha Msumbiji cha FRELIMO ameliambia bunge la nchi hiyo kuwa sheria hii iliyopasishwa inatoa fursa ya kuijenga upya Msumbiji na kuweka mbele maslahi ya nchi.
Nalo kundi la wabunge wa upinzani katika bunge la Msumbiji limeeleza kuwa sheria iliyoidhinisha inatoa dira kwa ajili ya mustakbali wenye matumaini.