Jeshi la Algeria laruhusiwa kuhudumu nje ya mipaka ya nchi hiyo
Jeshi la Algeria limeruhusiwa kuhudumu nje ya mipaka ya nchi hiyo kufuatia marakebisho yaliyofanyika katika katiba ya nchi hiyo.
Televisheni ya Algeria imetangaza kuwa sheria hiyo imeidhinishwa na Baraza la Serikali baada ya marekebisho ya katiba hiyo. Suala la kuanzisha Mahakama ya Katiba, kuainishwa Makamu wa Kwanza wa Rais na kuondolewa marufuku ya kuhudumu jeshi nje ya mipaka ya Algeria, ni kati ya masuala yenye umuhimu yaliyofanyiwa marekebisho katika katiba ya nchi hiyo.
Kipengee cha 208 cha katiba ya Algeria kinaeleza kuwa, mabadiliko yaliyofanywa katika katiba ya nchi hiyo yanapaswa kufikishwa katika Bunge la Taifa baada ya kuidhinishwa na serikali na kisha kupigiwa kura ya maoni.
Kura hiyo ya maoni imepangwa kufanyika mwezi Novemba mwaka huu.