Waalgeria wanapiga kura ya kupasisha katiba mpya inayobana kipindi cha rais
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i64360-waalgeria_wanapiga_kura_ya_kupasisha_katiba_mpya_inayobana_kipindi_cha_rais
Zaidi ya Waalgeria milioni 24 leo wanashiriki katika zoezi la kuipigia kura katiba mpya ya nchi hiyo inayobana kipindi cha uongozi wa rais wa nchi na kulipa Bunge la Mahakama mamlaka makubwa zaidi.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Nov 01, 2020 03:32 UTC
  • Waalgeria wanapiga kura ya kupasisha katiba mpya inayobana kipindi cha rais

Zaidi ya Waalgeria milioni 24 leo wanashiriki katika zoezi la kuipigia kura katiba mpya ya nchi hiyo inayobana kipindi cha uongozi wa rais wa nchi na kulipa Bunge la Mahakama mamlaka makubwa zaidi.

Hatua hiyo inakuja yapata mwaka mmoja baada ya kuchaguliwa Rais wa nchi hiyo, Abdelmadjid Tebboune, na miaka miwili baada ya kuanza harakati ya wananchi iliyomuondoa madarakani rais wa zamani wa nchi hiyo, Abdel Aziz Bouteflika.

Wakati wa kuapishwa kwake Disemba mwaka jana, Rais Abdelmadjid Tebboune aliahidi kufanya mabadiliko ya katiba akisisitiza kuwa, katiba mpya itapunguza madaraka ya rais na kukomesha utawala wa mtu mmoja.

Abdelmadjid Tebboune

Katiba mpya ya Algeria inasisitiza kuwa rais wa nchi atatawala kwa awamu zisizozidi mbili.

Katiba hiyo pia inalipa madaraka zaidi Bunge la Mahakama za Algeria, na vilevile inaliruhusu jeshi la nchi hiyo kutekeleza majukumu yake nje ya nchi; hii ikiwa ni mara ya kwanza kabisa katika historia ya nchi hiyo.