Eneo la Biashara Huru la Afrika, AfCFTA, laanza rasmi kazi
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i65530-eneo_la_biashara_huru_la_afrika_afcfta_laanza_rasmi_kazi
Eneo la Biashara Huru la Afrika, AfCFTA, limezinduliwa rasmi Januari Mosi 2021 ikiwa ni hatua kubwa katika kujumuisha soko la pamoja la nchi za Afrika.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jan 01, 2021 23:15 UTC
  • Eneo la Biashara Huru la Afrika, AfCFTA, laanza rasmi kazi

Eneo la Biashara Huru la Afrika, AfCFTA, limezinduliwa rasmi Januari Mosi 2021 ikiwa ni hatua kubwa katika kujumuisha soko la pamoja la nchi za Afrika.

Kwa soko la pamoja la zaidi ya watu bilioni 1.2 na Pato la Taifa la trilioni $2.5 AfCFTA inaweza kuifanya Afrika iwe na eneo huru la biashara kote duniani. 

Mwenyekiti wa zamu wa Umoja wa Afrika Bw. Cyril Ramaphosa, amesema kufikiwa kwa makubaliano ya biashara huria ya bara la Afrika AfCFTA ni muhimu katika hali ya sasa ya mfumo wa biashara ya pande nyingi kutishiwa. Amesema bila shaka eneo hilo litaboresha mustakabali wa Afrika kuwa mahali pa kuvutia uwekezaji.

Wamkele Mene Katibu Mkuu wa Idara ya Usimamizi wa Soko Huru la Bara Afrika anasema soko huru katika bara Afrika lilitarajiwa kuongeza biashara kati ya mataifa ya Afrika kutoka 18% hadi 50% ifikapo mwaka 2030.

Ameongeza ku,wa Waafrika wote wanayaona makubaliano haya, kama fursa ya kuufunua ukurasa mpya katika maendeleo ya kiuchumi ya Afrika, katika mwelekeo wa ukuaji. Aidha amesema mapatano hayo ni  ni fursa ya kipekee kwa Afrika ambayo haijawahi kupatikana tangu mwisho wa kipindi cha ukoloni.

Aidha amesema anadhamiria kuhakikisha kwamba mataifa yote ya Afrika, makubwa na madogo yananufaika kutokana na makubaliano haya.