Wanamgambo 10 wa Boko Haram waangamizwa na jeshi la Nigeria
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i70776-wanamgambo_10_wa_boko_haram_waangamizwa_na_jeshi_la_nigeria
Wanamgambo 10 wa kundi la kigaidi la Boko Haram wameangamizwa kwenye operesheni iliyoendeshwa na jeshi la Nigeria.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jun 01, 2021 03:47 UTC
  • Wanamgambo 10 wa Boko Haram waangamizwa na jeshi la Nigeria

Wanamgambo 10 wa kundi la kigaidi la Boko Haram wameangamizwa kwenye operesheni iliyoendeshwa na jeshi la Nigeria.

Msemaji wa jeshi la Nigeria, Mohammed Yerima amesema katika taarifa kwamba jeshi lilizuia jaribio la shambulizi la Boko Haram katika mkoa wa Rann, jimbo la Borno.

Akibainisha kuwa magaidi 10 waliuawa katika operesheni dhidi ya Boko Haram baada ya kuzuia shambulizi hilo, Yerima alisema kuwa magaidi wengi walikimbia wakiwa wamejeruhiwa. Yerima pia alisema kuwa silaha na idadi kubwa ya risasi pamoja na mali za magaidi zilikamatwa.

Katikati ya mwezi uliopita, Jeshi la Nigeria lilitangaza kuwa, limeua wanamgambo wasiopungua 9 wa Boko Haram baada ya wanamgambo hao kujaribu kufanya shambulio la uharibifu katika mji wa Maiduguri, makao makuu ya jimbo la Borno.

Maiti ya mmoja wa wananchama wa Boko Haram

Kwa makumi ya miaka sasa Nigeria imo vitani kupambana na mgaidi wa Boko Haram ambao wametangaza utiifu wao kwa genge la kigaidila Daesh (ISIS). 

Mgogoro wa Boko Haram umeshaua watu wasiopungua 36,000 na kusababisha mamilioni ya wengine kuwa wakimbizi ndani na nje ya Nigeria hasa katika maeneo yanayopakana na Ziwa Chad.