Russia: Tuko tayari kupatanisha mvutano kuhusu bwawa la Bwawa la Renaissance
Balozi wa Russia mjini Cairo, Misri amesisitiza kuwa usalama wa maji ni changamo kubwa kwa Misri na ni kadhia muhimu kwa nchi hiyo.
Giorgy Borisenko ametoa taaifa rasmi akieleza kuwa, Moscow inaelewa wasiwasi mkubwa wa nchi rafiki yake, Misri kuhusu ujenzi wa Bwawa la Renaissance. Amesema, Russia siku zote inasisitiza udharura wa kupatiwa ufumbuzi mzozo wa bwawa hilo kwa njia ya kiadilifu.
Balozi wa Russia huko Cairo ametilia mkazo pia kwamba nchi tatu jirani yaani Misri, Sudanna Ethiopia zinapasa kufanya juhudi za kufikia mapatano ya ufumbuzi wa suala hilo. Amesema Russia iko tayari kuwa mpatanishi katika mvutano wa Bwawa la Renaissance na iko tayari kufanya mazungumzo na Addis Ababa kuhusu suala hilo.
Mazungumzo ya pande tatu kati ya Misri, Ethiopia na Sudan chini ya usuluhishi wa Umoja wa Afrika hadi sasa yamegonga mwamba. Ujenzi wa Bwawa la Renaissance juu ya maji ya Mto Nile huko Ethiopia umeibua mvutano mkubwa wa maji kati ya nchi hizo tatu tangu mwaka 2011 hadi sasa.