Kituo cha upekuzi cha jeshi la Mali chashambuliwa na watu wasiojulikana
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i7624-kituo_cha_upekuzi_cha_jeshi_la_mali_chashambuliwa_na_watu_wasiojulikana
Duru za kijeshi za Mali zimetangaza habari ya kushambuliwa kituo kimoja cha upekuzi cha jeshi la nchi hiyo na watu wenye silaha.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
May 23, 2016 02:46 UTC
  • Kituo cha upekuzi cha jeshi la Mali chashambuliwa na watu wasiojulikana

Duru za kijeshi za Mali zimetangaza habari ya kushambuliwa kituo kimoja cha upekuzi cha jeshi la nchi hiyo na watu wenye silaha.

Duru za kijeshi za Mali zimetangaza kuwa, watu wenye silaha wasiojulikana wameshambulia kituo kimoja cha upekuzi cha jeshi la serikali katika eneo la kaskazini magharibi mwa nchi hiyo na kupelekea mwanajeshi mmoja kuuawa na wengine wanne kujeruhiwa, huku hali ya wawili kati yao ikiwa mahututi.

Duru za kijeshi za Mali zimeongeza kuwa, wanajeshi hao walikuwa wakilinda usalama wa shirika la Salam katika eneo lililoko umbali wa kilomita 20 kutoka mji wa Goundam, mkoani Timbuktu, kaskazini mwa Mali.

Wakati huo huo mwandishi wa shirika la habari la Mali ameripoti kutoka mkoani Timbuktu kwamba watu wasiojulikana wenye silaha wameshambulia gari moja iliyokuwa na mafundi wa shirika moja la simu katika eneo lililoko karibu na barabara kuu ya Goundam. Dereva wa gari hiyo amejeruhiwa vibaya huko kondakta wake akiwa hajulikani alipo hadi hivi sasa.