Shambulizi ya anga laua wafanyakazi 56 wa misaada ya kibinadamu Tigray
Shambulio la anga katika eneo la Tigray nchini Ethiopia limesababisha vifo vya watu 56 na kujeruhi wengine 30 wakiwemo watoto, katika kambi ya watu waliokimbia makazi yao. Hayo yamesemwa na wafanyakazi wawili wa kutoa misaada wakinukuu mamlaka za eneo hilo na watu walioshuhidia maafa hayo.
Wafanyakazi hao wa misaaada ya kibinadamu ambao hawakutaka majina yao yatajwe, wamesema shambulio hilo la anga lililolenga mji wa Dedebit, kaskazini-magharibi mwa eneo la karibu na mpaka na Eritrea, lilitokea Ijumaa usiku.
Wamesema kuwa idadi ya watu waliouawa katika shambulio hilo imedhibitishwa na maafisa wa utawala wa eneo hilo.
Mmoja wa wahudumu wa misaada aliyetembelea hospitali kuu ya Shire Suhul ambako majeruhi wamepelekwa kwa ajili ya matibabu, amesema kambi hiyo inawahifadhi vikongwe na watoto wengi.
Msemaji wa Jeshi la Ethiopia, Kanali Getnet Adane na msemaji wa Serikali Legesse Tulu wamekataa kujibu maswali ya waandishi wa habari kuhusu madai hayo.
Itakumbukwa kuwa, Disemba 30 mwaka jana Ofisi ya Uratibu wa Misaada ya Kibinadamu ya Umoja wa Mataifa iliripoti kuwa, makumi ya raia wameuawa katika mashambulizi ya anga kusini mwa eneo la Tigray. Umoja wa Mataifa uliyataja mauaji hayo ya raia kuwa mashambulizi makali zaidi kuwahi kuripotiwa tangu mwezi Oktoba mwaka jana.