Umoja wa Afrika wataka kusimamishwa mgogoro wa Ukraine
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i80762-umoja_wa_afrika_wataka_kusimamishwa_mgogoro_wa_ukraine
Umoja wa Afrika umetoa mwito wa kusimamishwa haraka iwezekanavyo mgogoro wa Ukraine.
(last modified 2025-10-20T07:03:11+00:00 )
Feb 25, 2022 14:47 UTC
  • Umoja wa Afrika wataka kusimamishwa mgogoro wa Ukraine

Umoja wa Afrika umetoa mwito wa kusimamishwa haraka iwezekanavyo mgogoro wa Ukraine.

Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika, ambaye pia ni Rais wa Senegal Macky Sall, pamoja na Mwenyekiti wa Kamisheni ya AU, Moussa Faki Mahamat wametangaza kusikitishwa kwao na vita baina ya Russia na Ukraine huko mashariki mwa Ulaya.

Taarifa ya viongozi hao iliyotolewa na Kamisheni ya AU imeitaka jamii ya kimataifa kuupatia ufumbuzi mgogoro huo kwa kuzingatia sheria za kimataifa na mamlaka ya kujitawala nchi nyingine.

Wakuu hao wa Umoja wa Afrika wamesisitiza kuwa, pande mbili kwenye mgogoro wa Ukraine na Russia zinapaswa kusitisha vita mara moja, na kufanya mazungumzo ya kisiasa pasi na kupoteza muda, chini ya uongozi wa Umoja wa Mataifa.

Vita vya Russia na Ukraine

Wasema mazungumzo hayo ya kisiasa yaitafanya dunia iondokane na matokeo hasi ya mgogoro huo, na kutatuliwa mgogoro huo ni kwa malashi ya amani na uthabiti wa watu wote duniani.

Jumatano asubuhi, Rais Vladimir Putin wa Russia alitangaza kuanza opereseheni maalumu dhidi ya Ukraine na kusema kuwa, operesheni hiyo inafanyika ili kuzuia kutokea vita vikubwa vya dunia na kuifanya Ukraine isiwe tishio la kijeshi kwa Russia.