Waislamu wa Gambia wanaoishi Marekani, waitaka Washington ikomeshe dhulma nchini mwao
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i8197-waislamu_wa_gambia_wanaoishi_marekani_waitaka_washington_ikomeshe_dhulma_nchini_mwao
Wanaharakati wa Kiislamu raia wa Gambia wanaoishi nchini Marekani, wameandamana hadi mbele ya ikulu ya White House wakitaka kuhitimishwa dhulma na ukandamizaji nchini mwao.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
May 31, 2016 11:04 UTC
  • Waislamu wa Gambia wanaoishi Marekani, waitaka Washington ikomeshe dhulma nchini mwao

Wanaharakati wa Kiislamu raia wa Gambia wanaoishi nchini Marekani, wameandamana hadi mbele ya ikulu ya White House wakitaka kuhitimishwa dhulma na ukandamizaji nchini mwao.

Kwa mujibu wa habari, maandamano hayo yaliyowashirikisha wanaharakati wa kisiasa wa Gambia nchini Marekani, yalifanyika jana Jumatatu ambapo walilalamikia hali mbaya ya haki za binaadamu na mwenendo wa serikali ya Gambia wa kuwakamata na kuwaweka kizuizini kwa makundi wapinzani wa kisiasa nchini humo. Waandamanaji hao waliokuwa wamebeba mabango yaliyokuwa na jumbe za "Gambia inahitaji msaada" na "Umoja ni Nguvu" wametaka pia kukomeshwa vitendo hivyo vya utiaji mbaroni huo wa kiwango kikubwa nchini. Mmoja wa waandamanaji alinukuliwa akisema kuwa, wanaharakati wa Kiislamu wa Gambia wanaoishi Marekani wameamua kufanya maandamano hayo ili kuuthibnitishia ulimwengu kwamba, Rais Yahya Jammeh wa nchi hiyo anatumia vibaya Uislamu katika kufikia malengo yake mabaya. Hii ni katika hali ambayo duru za habari nchini Gambia zinaeleza kuwa, hadi sasa idadi kadhaa ya masheikh wanaendelea kushikiliwa katika jela za nchi hiyo.