Misaada ya kibinadamu yatumwa kwa waathirika wa vita na njaa Ethiopia
Misaada ya kibinadamu kutoka Benki ya Dunia na Shirika la Kimataifa la Msalaba Mwekundu imeanza kuwafikia raia wa Ethiopia zaidi ya milioni sita waliathiriwa na vita na wanaokabiliwa na hatari ya njaa.
Maeneo ya Kaskazini mwa Ethiopia yamekumbwa na mapigano na hali ya mchafukoge tangu mwezi Novemba mwaka juzi. Waziri Mkuu wa nchi hiyo Abiy Ahmed, Novemba 4 mwaka juzi alitoa mari ya kutekelezwa mashambulizi katika maeneo ya Kaskazini mwa Ethiopia hususan katika eneo la Tigray baada ya kuwatuhumu wapiganaji wa Harakati ya Ukombozi wa Watu wa Tigray (TPLF) kuwa wamevishambulia vikosi vya serikali.
Mapigano huko Kaskazini mwa Ethiopia hadi sasa yamesababisha watu karibu milioni mbili kuwa wakimbizi na kuwalazimisha wengine laki nne kukabiliwa na ukosefu wa chakula.
Msafara wa magari yaliyobeba misaaada mbalimbali ya kibinadadamu umeonekana ukielekea katika maeneo ya Kaskazini mwa Ethiopia hususan katika jimbo la Tigray baada ya kusitishwa kwa siku kadhaa.
Wakati huo huo Mpango wa Chakula wa Umoja wa Mataifa (WFP) umetangaza kuwa, malori 47 ya shirika hilo yaliyosheheni bidhaa mbalimbali za chakula yameleeka Tigray.
Serikali ya Ethiopia imetangaza kwamba itashirikiana na jumuiya ya kimataifa kufikisha misaada kwa wananchi na imewataka waasi kuondoka haraka iwezekanavyo katika maeneo ya Tigris na Afar ili kutoa huduma bora za misaada kwa waliokimbia makazi yao.