Katibu Mkuu wa UN atiwa wasiwasi na maandamano Libya
Antonio Guterres Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema ana wasiwasi na maandamano ya wananchi yaliyoshuhudiwa hivi karibuni katika miji kadhaa huko Libya ya kulalamikia hali mbaya ya maisha.
Libya imeathiriwa na machafuko na uksoefu wa amani tangu kupinduliwa kiongozi wa nchi hiyo Kanali Muammar Gaddafi mwaka 2011 kwa uingliaji wa nchi ajinabi. Jamii ya kimataifa na Umoja wa Mataifa zinaamini kuwa njia pekee ya kuupatia ufumbuzi mgogoro wa Libya ni kufanyika chaguzi za rais na bunge nchini humo.
Antonio Guterres Katibu Mkuu wau Umoja wa Mataifa jana Jumapili alisema anatiwa wasiwasi na maandamano yaliyoshudhudiwa hivi karibuni katika miji kadhaa nchini Libya na kutaka kutambuliwa rasmi haki ya wananchi ya kuandamana kwa amani. Wakati huo huo Guterres amewatolea wito wananchi wa Libya kufanya maandamano kwa amani na kujiepusha na machafuko.
Wakati huo huo Stephen Williams Mshauri Maalumu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika Masuala ya Libya juzi Jumamosi alitaka kuheshimiwa haki ya wananchi wa Libya ya kuandamana kwa amani na kusema anapinga ghasia na utumiaji mabavu nchini humo. Ijumaa iliyopita wananchi wa Libya waliandamana mkababa wa bunge la taifa la nchi hiyo huko Tobruk wakilalamikia hali ngumu ya maisha. Wafanya maandamano hao kisha waliingia ndani ya bunge na kuchoma moto baadhi ya nyaraka rasmi walizokuta humo.
Mji wa Benghazi pia ulikumbwa na maandamano kama hayo ambapo waandamanaji walitaka kujiuzulu baraza la uongozi, bunge na serikali za al Dbaibeh na al Bashaga.