Vituo viwili vya afya vyashambuliwa kaskazini magharibi mwa Nigeria
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i89452-vituo_viwili_vya_afya_vyashambuliwa_kaskazini_magharibi_mwa_nigeria
Majambazi waliokuwa na silaha wameshambulia hospitali na kituo cha afya huko kaskazini magharibi mwa Nigeria na kuua watu kadhaa.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Oct 19, 2022 07:02 UTC
  • Vituo viwili vya afya vyashambuliwa kaskazini magharibi mwa Nigeria

Majambazi waliokuwa na silaha wameshambulia hospitali na kituo cha afya huko kaskazini magharibi mwa Nigeria na kuua watu kadhaa.

Katika miaka ya hivi karibuni Nigeria imekuwa ikikumbwa na mashambulizi ya umwagaji damu yanayotekelezwa na makundi ya kigaidi kama Boko Haram na magenge ya majambazi. 

Kituo cha polisi cha jimbo la Niger kaskazini magharibi mwa Nigeria kimethibitisha kutokea mashambulio hayo jana Jumanne kwenye hospitali ya serikali.

Wakazi wa eneo hilo wanasema, watu waliokuwa na silaha walivamia hospitali hiyo na kuiteketeza kwa moto. Watu wawili wameuawa katika hujuma hiyo.

Washambuliaji pia walichukua mateka karibu watu 20, ikiwa ni pamoja na idadi kubwa ya wafanyakazi na madaktari wa hospitali hiyo. 

Baadaye majambazi hao walishambulia kituo kingine cha afya katika eneo hilo. 

Jumuiya ya Madaktari Wasio na Mipaka imetoa taarifa ikilaani shambulio la kundi lenye silaha dhidi ya kituo cha afya katika eneo la Gomi jimboni Zamfara huko kaskazini-magharibi mwa Nigeria na kutangaza kuwa kitendo hicho hakikubaliki.