Juhudi za kuandaa sheria na kufanyika uchaguzi nchini Libya
Kufanyika uchaguzi nchini Libya na kuingia madarakani serikali yenye ridhaa ya wananchi na kwa mujibu wa mchakato wa demokrasia ndio takwa kuu na la kimsingi la wananchi wa nchi hiyo ya kaskazini mwa Afrika.
Hatua hiyo inatajwa na weledi wa mambo kuwa, njia bora kabisa ya kuhitimisha mgogoro wa kisiasa wa nchi hiyo ambayo imeendelea kuandamwa na jinamizi la machafuko tangu kuangushwa utawala wa Kanali Muammar Gaddafi.
Katika kufikia lengo hilo, baada ya mazungumzo ya vuta nikuvute yaliyodumuu kwa muda sasa, hatimaye kumefikiwa mwafaka wa namna ya unavyopaswa kuwa mfumo wa kisiasa wa nchi hiyo. Khalid al-Mishri, Mkuu wa Baraza Kuu la Serikali ya Libya sambamba na kuashiria kwamba, katika mfumo ujao wa nchi hiyo ili kuleta uwiano wa kisiasa, Bunge litaundwa na mabaraza mawili amesema: Makao ya Bunge yatakuwa katika mji wa Benghazi na Baraza la Seneti makao yake makuu yatakuwa katika mji mkuu Tripoli.
Kwa mujibu wa waraka wa makubaliano hayo ni kuwa, serikali itakuwa ni mjumuiko wa Rais na baraza la mawaziri na kwamba, Rais ndiye atakayemteua Waziri Mkuu. Aidha kwa mujibu wa waraka huo, mtu yeyote ambaye amewahi kukabiliwa na hukumu ya mahakama hana haki ya kugombea urais. Kadhalika shakhsai wenye nyadhifa za kijeshi na zisizo za kijeshi wanapaswa kuuiuzulu nyadhifa zao kabla ya kujiandikisha kwa ajili ya kugombea kiti cha urais.
Hata kama nukta za kina katika yale yaliyko ndani ya waraka huo hazijatangazwa rasmi na bayana, lakini hilo linaweza kutathminiwa kama hatua moja mbele kwa ajili ya kufanyika uchaguzi wa Libya. Disemba mwaka jana (2021) Libya ilishindwa kufanyya uchaguzi kama ilivyokuwa imepangwa kutokana na kushaididi mivutano na vyama vya siasa kushindwa kufikia mwafaka wa sheria za uchaguzi.
Libya yenye utajiri wa mafuta imekumbwa na machafuko tangu 2011 wakati mtawala wa muda mrefu Muammar Gaddafi alipong'olewa madarakani baada ya kukaa madarakani kwa miongo minne.
Hali imekuwa mbaya zaidi tangu mwezi Machi mwaka jana wakati Bunge lenye makao yake Mashariki mwa Libya lilipoteua serikali mpya inayoongozwa na aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani Fathi Bashagha, lakini Waziri Mkuu wa serikali ya Tripoli, Abdul Hamid Dbeibeh, mmoja wa watu wawili wanaodai kuwa ndio watawala wastahiki nchini Libya, anasisitiza kuwa atakabidhi madaraka kwa serikali inayoingia madarakani kupitia "bunge lililochaguliwa na wananchi," na hivyo kuzua hofu kwamba Libya inaweza kurejea katika vita vya wenyewe kwa wenyewe.
Muhammad al-Manfi, Mkuu wa Baraza la Uongozi la Libya anasema: Utatuzi wa mgogoro wa Libya unaweza kupatikana tu kupitia njia ya kuhuisha roho ya kiraifa, kufidia hasara na kurejea katika hekima na busara.
Ukweli wa mambo ni kuwa, makundi ya Libya yanafanya hima kuhitimisha mgogoro na mkwamo wa kisiasa wa nchi hiyo ambao umedumu kwa karibuu miaka 12 tangu kuangushwa utawala wa kanali Muammar Gaddafi.
Filihali hali ya mambo nchini Libya imegeuka na kuwa daghadagha kuu kwa wachezaji wote wakuu wa kisiasa hasa kwa kutilia maanani anga ya kisiasa inayotawala hivi sasa, kuongezeka hatari ya uwepo wa madola ya kigeni na kila mmoja kutaka hisa yake huko Libya na vile vile kuongezeka harakati za makundi yya kigaidi.
Inaonekana kuwa, kwa mara nyingine tena Libya imekaribia kufanya uchaguzi. Licha ya kuwa yumkini kama ilivyokuwa hapo kabla kukashuhuudiwa tena ukwamishaji mambo na hivyo kupelekea uchaguzi huo kuakhirishwa, lakini ukweli wa mamboi ni kuwa, hivi sasa hali ya Libya ni mbaya mno kiasi kwamba, imefikia hatua ya kutaka kugawanyika.