Algeria: Palestina itaendelea kuwa kadhia kuu ya Ulimwengu wa Kiislamu
Rais wa Algeria amesema kukwa, Palestina itaendelea kuwa kadhiaa kuu ya Ulimwengu wa Kiislamu na Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu OIC.
Algeria imekuwa mtetezi wa haki za wananchi wa Palestina muda wote na imekuwa ikiunga mkono kadhia ya Quds kwa njia mbalimbali.
Kwa mujibu wa IRNA, Rais Abdel Majid Taboun wa Algeria amesema hayo usiku wa kuamkia leo Jumatatu katika kikao cha Umoja wa Mabunge ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu OIC, kilichofanyika nchini Algeria, na kueleza kuwa, Palestina itaendelea kuwa nchi na suala kuu la Umma wa Kiislamu na OIC. Vile vile ametaka juhudi ziongezwe maradufu kuwasaidia Wapalestina katika mapambano yao ya kukabiliana na jinai za utawala ghasibu wa Kizayuni.
Rais Abdel Majid Taboun pia amesema, Algeria itashirikiana na nchi za Kiislamu na Waislamu duniani kote kwa ajili ya kukhakikisha kuwa Palestina inakuwa mwanachama kamili wa Umoja wa Mataifa.
Kabla ya hapo Rais huyo wa Algeria aliyataka mataifa ya dunia kuchukua hatua za kivitendo za kuunga mkono haki za wananchi wa Palestina na kusisitiza kuwa, uungaji mkono huo haupaswi kuwa na msururu wa kauli na maneno tu.
Haki za wananchi madhulumu wa Palestina zinakandamizwa na utawala ghasibu wa Kizayuni wa Israel unaofanya jinai za kutisha dhidi ya Wapalestina kwa kwa zaidi ya miaka sabini sasa.