Uganda yaitaka Kenya kutofunga kambi ya wakimbizi ya Dadaab
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i9898-uganda_yaitaka_kenya_kutofunga_kambi_ya_wakimbizi_ya_dadaab
Serikali ya Uganda imeitaka Kenya kuangalia upya uamuzi wake wa kufunga kambi ya wakimbizi ya Dadaab nchini humo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jun 24, 2016 23:55 UTC
  • Uganda yaitaka Kenya kutofunga kambi ya wakimbizi ya Dadaab

Serikali ya Uganda imeitaka Kenya kuangalia upya uamuzi wake wa kufunga kambi ya wakimbizi ya Dadaab nchini humo.

Hayo yamesemwa na Hillary Onek, Waziri wa Misaada na Kukabiliana na Majanga wa nchini Uganda katika moja ya sherehe zilizofanyika kusini mwa nchi hiyo ambapo aliwataka viongozi wa nchi jirani ya Kenya kuangalia upya suala hilo la kufungwa kwa kambi za wakimbizi za Dadaab na Kakuma kaskazini mashariki mwa Kenya ambazo ndani yake wanaishi wakimbizi wa Somalia. Amesema kuwa ni suala la dharura kuangaliwa upya uamuzi huo kabla ya kutekelezwa kutokana na athari zake za baadaye. Kambi ya wakimbizi ya Dadaab ina karibu wakimbizi laki sita ambao aghlabu yao ni raia wa Somalia. Viongozi wa Kenya wametangaza azma yao ya kuzifunga kambi hizo ifikapo mwezi Mei mwaka kesho kutokana na matatizo ya kiuchumi, mazingira na usalama. Wakati huo huo Apollo Kazungu, kamishna wa masuala ya wakimbizi katika ofisi ya waziri mkuu nchini Uganda, ameitaka serikali ya nchi hiyo na nchi zingine kufanya mawasiliano ya simu na viongozi wa Nairobi, kwa lengo la kuwashawishi kuangalia upya uamuzi wao huo.