William Ruto: Kenya ina akiba ya kutosha ya chakula
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i9958-william_ruto_kenya_ina_akiba_ya_kutosha_ya_chakula
Naibu Rais wa Kenya amekanusha madai na uvumi kwamba, nchi hiyo ya Afrika Mashariki inakabiliwa na uhaba mkubwa wa chakula.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jun 25, 2016 11:04 UTC
  • William Ruto: Kenya ina akiba ya kutosha ya chakula

Naibu Rais wa Kenya amekanusha madai na uvumi kwamba, nchi hiyo ya Afrika Mashariki inakabiliwa na uhaba mkubwa wa chakula.

William Ruto amesema kuwa, madai kwamba, Kenya inakabiliwa na uhaba mkubwa wa chakula hayana msingi wowote ni uvumi mtupu. Naibu Rais wa Kenya amebainisha kwamba, maghala ya kiistratejia ya chakula ya nchi hiyo yana akiba ya kutosha ya chakula. Amesema maghala hayo yamejaa mahindi ya akiba ambayo yanaweza kutumiwa mpaka katika msimu wa mavuno hivyo hakuna haja ya kutiwa wasiwasi na uvumi wa upungufu wa chakula unaoenezwa na baadhi ya watu.

William Ruto amewataka watu wanaoeneza uvumi huo baina ya watu kwa ajili ya kufikia malengo yao kuacha kufanya hivyo mara moja kwani wana imani na serikali kuhusiana na suala la kuweko akiba ya kutosha ya chakula.

Uvumi kuhusiana na kuweko upungufu wa chakula nchini Kenya ulianza baada ya Taasisi ya Nafaka ya nchi hiyo kutahadharisha kuhusiana na uhaba wa mahindi nchini humo na kupanda kwa bei ya unga wa mahindi katika siku za usoni.