-
Mgogoro wa Pakistan na matokeo mabaya ya kuhukumiwa maafisa 15 wa jeshi
Jun 29, 2023 23:57Msemaji wa jeshi la Pakistan, Jenerali Ahmed Sharif Chaudhry amesema kuwa, maafisa 15 wa jeshi hilo wametiwa mbaroni wakihusishwa na machafuko yaliyotokewa baada ya kukamatwa waziri mkuu wa zamani wa nchi hiyo, Imran Khan.
-
Vikwazo ni sawa na silaha ya kivita
Jun 29, 2023 03:54Katibu wa Kamati ya Haki za Binadamu ya Idara ya Mahakama ya Iran amesema kuwa, vikwazo ni jinai kubwa dhidi ya binadamu na kwamba Marekani ndiye mtendaji mkuu wa jinai hiyo kutokana na uraibu wake wa kuziwekea vikwazo nchi nyingine bila ya sababu ya maana.
-
Kioja cha karne; si ubaguzi, bali ni sadfa polisi wa Ufaransa kuua Waislamu na watu weusi tu!
Jun 28, 2023 22:59Jumanne jioni, Juni 27, 2023, polisi wa Ufaransa walimpiga risasi na kumuua kijana mdogo Mfaransa mwenye umri wa miaka 17 tu mwenye asili ya Algeria katika kituo cha ukaguzi huko Marseille. Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron imemchukua muda kuchakachua la kusema hadi jana Jumatano na baada ya kutokea fujo kubwa zilizotokana na hasira kubwa za wananchi. Macron ameishia kusema tu kuwa amesikitishwa na mauaji hayo na kuwataka wananchi wasikarike na watulie.
-
Kuzidi kuporomoka nafasi ya Netanyahu huko Israel
Jun 27, 2023 22:51Matokeo ya uchunguzi wa maoni ya hivi karibuni kabisa uliofanywa na vyombo vya habari vya utawala ghasibu wa Israel yanaonyesha kuwa, mapenzi na uungaji mkono kwa Benjamin Netanyahu unazidi kuporomoka huku vyama tanzu katika serikali yake vikizidi kumuacha mkono.
-
Kuendelea ujenzi wa vitongoji haramu vya Israel licha ya kuweko upinzani mkubwa
Jun 27, 2023 09:24Utawala ghasibu wa Israel umeafiki mpango wa ujenzi wa nyumba mpya 5,623 katika Ukingo wa Magharibi ikiwa ni muendelezo wa mkakati wa kupora na kukalia kwa mabavu ardhi za Palestina.
-
Sababu zilizotolewa na Taliban kuhusu kutoruhusu kusoma wasichana wa Afghanistan
Jun 26, 2023 23:16Zabihullah Mujahid, msemaji wa kundi la Taliban la Afghanistan amesema kuwa, kuzuiwa wasichana nchini humo, kusoma masomo ya zaidi ya darasa la sita ni jambo la dharura kwa hivi sasa hadi pale vitabu vya masomo vitakapofanyiwa marekebisho.
-
Mapatano baina ya Kremlin na kundi la Wagner kwa upatanishi wa Aleksandr Lukashenko
Jun 26, 2023 12:01Hatimaye na katika kipindi cha chini ya siku moja, uasi wa kundi la wanamgambo wa Wagner linaloongozwa na Yevgeny Prigozhin umemalizika kwa upatanishi wa Rais Aleksandr Lukashenko wa Belerus.
-
Kukosoa China vigezo vya kindumakuwili katika kukabiliana na ugaidi
Jun 25, 2023 08:55Zhang Jun, balozi na mwakilishi wa China katika Umoja wa Mataifa amekosoa vikali vigezo vya kindumakuwili vya Marekani kuhusiana na suala la kukabiliana na ugaidi na kueleza kwamba, ugaidi bado ni changamoto muhimu ambayo inatishia amani na usalama wa kimataifa.
-
Mwakilishi wa Umoja wa Ulaya akiri kuhusu mauaji yasiyo na mfano wake dhidi ya Wapalestina
Jun 24, 2023 23:07Sven Kühn von Burgsdorff, mwakilishi wa Umoja wa Ulaya huko Palestina, amesema mauaji ya karibuni dhidi ya Wapalestina yalikuwa hayajawahi kuonekana tangu mwaka 2005 na kuongeza kuwa kile walichokifanya walowezi katika kijiji cha Tarmsaiya ni cha kigaidi.
-
Russia yapinga kushiriki Macron katika mkutano wa BRICS
Jun 24, 2023 07:13Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia, Sergei Ryabkov alitangaza Alhamisi iliyopita kwamba Moscow haidhani kuwa Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron, ataruhusiwa kuhudhuria mkutano ujao wa kundi la BRICS nchini Afrika Kusini, kwa sababu Paris inatekeleza sera ya chuki dhidi ya Moscow.