-
Kuanzisha uchunguzi Polisi ya Ujerumani dhidi ya Rais wa Palestina kuhusiana na Holocaust; undumakuwili mwingine wa Magharibi
Aug 21, 2022 03:50Polisi ya Ujerumani imesema, imeanzisha uchunguzi dhidi ya Mahmoud Abbas, Rais wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina kwa sababu ya kauli aliyotoa kuhusu Holocaust, yaani mauaji ya halaiki ya Wayahudi yanayodaiwa kufanywa na utawala wa Kinazi wa Ujerumani chini ya uongozi wa Adolf Hitler.
-
Vita vya Ukraine na kuongezeka vibaya mgogoro wa kiuchumi barani Ulaya
Aug 20, 2022 22:07Hali mbaya ya kiuchumi barani Ulaya inazidi kuwa mzigo mkubwa zaidi na zaidi kwa kadiri siku zinavyopita kiasi kwamba, mfumuko wa bei nchini Uingereza umepanda kwa asilimia 10 ikiwa ni mara ya kwanza tangu mwaka 1982 huku Waziri Mkuu wa Sweden akizungumzia uchumi za enzi za vita barani Ulaya.
-
Wapinzani Tunisia waendelea kupinga katiba mpya
Aug 20, 2022 09:04Wakati Rais wa Tunisia Kais Saied ametangaza kutekelezwa kwa katiba mpya ya nchi, Harakati ya Ennahda ya Tunisia imepinga hatua hiyo na kusema katiba hiyo haina uhalali. Harakati ya Ennahda imetangaza katiba mpya kama jaribio la kuhalalisha mapinduzi dhidi ya katiba, na pia ni dhidi ya mafanikio ya mwamko wa wananchi.
-
Kiwewe cha Marekani kwa kuzidi kuongezeka nguvu za China
Aug 19, 2022 22:11Marekani ambayo imeingia kiwewe kutokana na kuzidi kuongezeka nguvu za China, imeahidi kuchukua hatua za kukabiliana na Beijing katika kipindi cha wiki na miezi ijayo karibu na kisiwa cha Taiwan, kwa tamaa ya kupunguza kasi ya nguvu za kijeshi na kiuchumi za China.
-
Kuuawa Mawlawi Mehdi Mujahid, kamanda wa zamani wa Taliban kwa kulipinga kundi hilo
Aug 19, 2022 04:47Wizara ya Ulinzi ya Taliban nchini Afghanistan imetangaza habari ya kuuawa Mawlawi Mehdi Mujahid, kamanda wa zamani wa kundi hilo kutoka kabila la Hazara na ambaye alikuwa haridhishwi na utendaji wa kundi hilo. Kamanda huyo ameuawa kwa kupigwa risasi na Taliban huko Herat, magharibi mwa Afghanistan.
-
Mazungumzo ya vyama; njia ya kuikwamua Iraq katika mgogoro
Aug 18, 2022 22:10Rais, Waziri Mkuu na Spika wa Bunge pamoja na vyama kadhaa vya siasa vya nchi hiyo wametoa taarifa wakisisitizia ulazima wa kukomeshwa aina yoyote ile ya mzozo na mvutano katika mitaa na barabara za nchi hiyo.
-
Kufanyika kikao cha Kamisheni ya Pamoja ya Kiuchumi ya Iran na Pakistan mjini Islamabad
Aug 18, 2022 03:52Kikao cha 21 cha Kamisheni ya Pamoja ya Kiuchumi ya Iran na Pakistan kilianza Jumatano ya jana katika mji mkuu wa Pakistan Islamabad ambapo ujumbe wa Iran katika kikao hicho unaongozwa na Rostam Qassemi, Waziri wa Barabara na Ujenzi wa Miji.
-
Tamko la Putin kuhusu utayari wa Russia wa kuwapatia waitifaki wake silaha za kisasa kabisa
Aug 17, 2022 22:14Rais Vladimir Putin wa Russia amesema, Moscow iko tayari kuwapatia waitifaki wake wa Amerika ya Latini, Asia na Afrika aina mbalimbali za silaha za kisasa kabisa.
-
Jibu la Iran kwa rasimu iliyopendekezwa na Umoja wa Ulaya
Aug 17, 2022 04:45Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imekabidhi kwa mratibu wa Umoja wa Ulaya katika mazungumzo ya uondoaji vikwazo jibu la maandishi kuhusiana na nakala rasmi ya rasimu ya mapatano ya Vienna.
-
Iraq katika mkondo wa kushtadi zaidi mkwamo wa kisiasa
Aug 16, 2022 22:04Uamuzi wa makundi na mirengo ya kisiasa ya Iraq wa kufanya mikusanyiko ya barabarani umeifanya anga ya kisiasa ya nchi hiyo kuwa tete zaidi na mkwamo wa kisiasa unaoikabili nchi hiyo kushtadi zaidi.