Belarusi: Tuna azma thabiti ya kupanua ushirikiano wetu na Iran
https://parstoday.ir/sw/news/daily_news-i132580-belarusi_tuna_azma_thabiti_ya_kupanua_ushirikiano_wetu_na_iran
Waziri wa Mambo ya Nje wa Belarus amefanya mazungumzo na Naibu Waziri na Mkuu wa Kituo cha Utafiti wa Kisiasa na Kimataifa cha Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Iran na kusisitiza nia na azma thabiti ya nchi yake ya kupanua ushirikiano na Iran.
(last modified 2025-10-30T05:44:25+00:00 )
Oct 30, 2025 05:41 UTC
  • Saeed Khatibzadeh, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran na Maxim Ryzhenkov Waziri wa Mambo ya Nje wa Belarusi
    Saeed Khatibzadeh, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran na Maxim Ryzhenkov Waziri wa Mambo ya Nje wa Belarusi

Waziri wa Mambo ya Nje wa Belarus amefanya mazungumzo na Naibu Waziri na Mkuu wa Kituo cha Utafiti wa Kisiasa na Kimataifa cha Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Iran na kusisitiza nia na azma thabiti ya nchi yake ya kupanua ushirikiano na Iran.

Maxim Ryzhenkov ameashiria safari yenye mafanikio ya Masoud Pezzekian, Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran huko Minsk na kusisitiza nia ya dhati ya Belarus ya kustawisha na kuimarisha uhusiano na Tehran katika nyanja mbalimbali.

Katika mazungumzo yake na Saeed Khatibzadeh, Waziri wa Mambo ya Nje wa Belarusi amesema: Safari ijayo ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran mjini Minsk, ziara ya Rais wa Belarus mjini Tehran, kufuatilia na kukamilisha baadhi ya miradi ya pamoja katika uga wa njia za usafiri na mawasiliano ni masuala muhimu katika ajenda ya uhusiano wa pande mbili.

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran ambaye alikwenda Minsk kushiriki katika Mkutano wa Kimataifa wa Usalama wa Eurasia, pia ameashiria katika mazungumzo hayo umuhimu wa kuimarishwa uhusiano kati ya Iran na Jamhuri ya Belarus na kusema: Utashi wa Jamhuri ya Kiislamu ni kuendeleza na kupanua uhusiano wa kina na Jamhuri ya Belarusi na kuondoa vikwazo vyovyote katika mchakato huu.

Akigusia umuhimu wa uhusiano wa kistratijia kati ya nchi hizo mbili, Khatibzadeh alieleza matumaini yake kuwa, kwa kufanyika kikao kamisheni ya pamoja ya kiuchumi kati ya Iran na Belarus mjini Tehran, kubadilishana wajumbe wa ngazi za juu, na kutia saini makubaliano ya ushirikiano wa kimkakati kati ya nchi hizo mbili, tutashuhudia kuimarika kwa ushirikiano kati ya pande hizo mbili.