Zaidi ya Wapalestina 9,000 wanashikiliwa katika jela za Israel
https://parstoday.ir/sw/news/daily_news-i132834-zaidi_ya_wapalestina_9_000_wanashikiliwa_katika_jela_za_israel
Taasisi tatu za Palestina zinazohusiana na masuala ya mateka zimetangaza kuwa, utawala wa Israel unawashikilia Wapalestina 9,250 katika jela zake.
(last modified 2025-11-05T19:04:51+00:00 )
Nov 05, 2025 19:03 UTC
  • Zaidi ya Wapalestina 9,000 wanashikiliwa katika jela za Israel
    Zaidi ya Wapalestina 9,000 wanashikiliwa katika jela za Israel

Taasisi tatu za Palestina zinazohusiana na masuala ya mateka zimetangaza kuwa, utawala wa Israel unawashikilia Wapalestina 9,250 katika jela zake.

Shirika la Masuala ya Wafungwa na Watu Wanaoachiwa huru, Klabu ya Wafungwa wa Palestina, na Taasisi ya Masuala ya Wafungwa na Haki za Kibinadamu "Al-Dhameer" zilitangaza katika taarifa ya pamoja, kulingana na data ya Utawala wa kizayuni wa Israel ni kuwa,  hadi Novemba 2025, idadi ya mateka katika jela za utawala huo imezidi 9,250.

Miongoni mwa wafungwa hao, 49 ni wanawake na 350 ni watoto.