Idadi ya wahanga wa mashambulizi ya Pakistan nchini Afghanistan yaongezeka
https://parstoday.ir/sw/news/daily_news-i133988-idadi_ya_wahanga_wa_mashambulizi_ya_pakistan_nchini_afghanistan_yaongezeka
Idadi ya watu waliouawa na kujeruhiwa katika mashambulio ya Pakistan kwenye mkoa wa Kandahar nchini Afghanistan imeongezeka na kufikia watu 10.
(last modified 2025-12-06T12:43:13+00:00 )
Dec 06, 2025 12:25 UTC
  • Idadi ya wahanga wa mashambulizi ya Pakistan nchini Afghanistan yaongezeka

Idadi ya watu waliouawa na kujeruhiwa katika mashambulio ya Pakistan kwenye mkoa wa Kandahar nchini Afghanistan imeongezeka na kufikia watu 10.

Duru za hospitali za mkoa wa Kandahar zimesema kuwa, mashambulizi yaliyofanywa na jeshi la Pakistan katika mji wa Spin Boldak huko Kandahar yameua watu watano na kujeruhiwa huku mmoja waliouawa akiwa ni mtoto mdogo.

Abdullah Farooq, msemaji wa polisi wa mpakani wa Afghanistan amethibitisha habari hiyo na kusema kuwa, mashambulizi hayo ya Pakistan yamewalazimisha wanajeshi wa Afghanistan kujibu mashambulizi.