Israel yaendelea kushambulia Ghaza na Ukingo wa Magharibi
https://parstoday.ir/sw/news/daily_news-i134320-israel_yaendelea_kushambulia_ghaza_na_ukingo_wa_magharibi
Pars Today- Ndege za kivita na mizinga ya Israel kwa mara nyingine tena imeshambulia maeneo mbalimbali ya Ghaza, na wakati huo huo utawala huo katili umefanya mashambulizi makubwa katika Ukingo wa Magharibi dhidi ya wananchi wa Palestina.
(last modified 2025-12-15T07:01:04+00:00 )
Dec 15, 2025 06:24 UTC
  • Israel yaendelea kushambulia Ghaza na Ukingo wa Magharibi

Pars Today- Ndege za kivita na mizinga ya Israel kwa mara nyingine tena imeshambulia maeneo mbalimbali ya Ghaza, na wakati huo huo utawala huo katili umefanya mashambulizi makubwa katika Ukingo wa Magharibi dhidi ya wananchi wa Palestina.

Mizinga na ndege hizo za kivita za Israel zimeendelea kushambulia maeneo mbalimbali ya Ghaza, ikiwa ni pamoja na Jiji la Ghaza upande wa mashariki, Khan Yunis na kambi ya wakimbizi ya Al-Bureej. Meli za kivita za Israel pia zimefyatua risasi kwenye maeneo ya pwani ya Ghaza.

Vyanzo vya ndani viliripoti kuzorota kwa hali ya kibinadamu katika kambi za wakimbizi kutokana na mvua kubwa na uharibifu wa mahema.

Wakati huo huo, baraza la mawaziri la Israel limekataa kuingia katika awamu ya pili ya mazungumzo ya kusitisha mapigano, likitumia kisingizio cha mwili wa mfungwa wa Kizayuni. Lakini Muqawama wa Palestina umetangaza kwamba shughuli za utafutaji zinaendelea katika hali ngumu.

Wakati huo huo, vikosi vya dola vamizi la Kizayuni vimevamia maeneo mbalimbali ya Ukingo wa Magharibi, ikiwa ni pamoja na Jenin, Jaba, Aqaba Jabr, Deir Jarir, Beit Rima na Nablus, na kuwateka nyara Wapalestina kadhaa na kuwapeleka kusikojulikana.