Amir- Abdollahian: Maneno na vitisho vya utawala bandia wa Kizayuni havina nafasi
(last modified Mon, 25 Sep 2023 04:45:01 GMT )
Sep 25, 2023 04:45 UTC

Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza kuwa hii leo Wazayuni wamedhoofika pakubwa na hakuna anayebabaishwa na vitisho vya utawala huo.

Hossein Amir Abdollahian ambaye alielekea New York kwa lengo la kushiriki katika Mkutano wa 78 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (UNGA) amesema mbele ya waandishi wa habari Wairani kuhusu vitisho vya Waziri Mkuu wa utawala wa Kizayuni kwamba: Benjamin Netanyahu na utawala bandia wa  Kizayuni si chochote si lolote na kama wangeweza kufanya jambo lolote, basi wasingetumia lugha na mbinu ya vitisho kama hii. 

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran ameongeza kuwa Wazayuni leo hii wanakabiliwa na migogoro ya matabaka kadhaa ndani ya ardhi zinazokaliwa kwa mabavu. Amir Abdollahian aidha amebainisha kuwa, Waziri Mkuu wa utawala bandia na ghasibu badala ya kuheshimu sheria na umoja wa Mataifa anatumia kongamano hilo kutoa vitisho, na hii inaonyesha namna utawala wa Kizayuni unavyotumia vibaya vyombo vya kimataifa. 

Amir Abdollahian ameashiria pia mazungumzo aliyofanya na Antonio Guterres Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa huko New York na kusema: Katika sehemu moja ya mazungumzo yao waligusia pia ubunifu na pendekezo lililotolewa na Rais Sayyid Ebrahim Raisi kuhusu udharura wa kufungamana na kushikamana na mhimili wa  familia.

Amir Abdollahian na Katibu Mkuu wa UN, Antonio Guterres mjini New York