MAHOJIANO na mwanahabari wa Kenya aliyeshiriki Tamasha la Khorshid Iran
(last modified Tue, 03 Oct 2023 15:03:01 GMT )
Oct 03, 2023 15:03 UTC
  • MAHOJIANO na mwanahabari wa Kenya aliyeshiriki Tamasha la Khorshid Iran

Mji wa pili kwa ukubwa nchini Iran wa Mashhad hivi karibuni ulikuwa mwenyeji wa mkutano muhimu wa waandishi wa habari wanawake mashuhuri wanaofanya kazi katika majukwaa mbadala ya vyombo vya habari kutoka kote ulimwenguni.

Jumla ya waandishi wa habari wanawake 100 kutoka zaidi ya nchi 40 walijumuika pamoja kwa ajili ya tamasha hilo na kubadilishana tajiriba na mawazo yao juu ya matukio ambayo ni nadra kutangazwa na vyombo vya habari vya kawaida.

Mada zilizojadiliwa wakati wa tamasha hilo la siku tatu ni pamoja na wanawake katika vyombo vya habari na kukuza haki ya kijamii, taasisi ya familia chini ya mashambulizi ya vyombo vya habari, wanawake na vyombo vya habari vya muqawama au mapambano, jukumu la vyombo vya habari katika kurekebisha ukatili dhidi ya wanawake na vyombo vya habari na utumwa wa kisasa. Radio Tehran imezungumza na mmoja wa washiriki wa mkutano huo kutoka Kenya…..