Wamorocco: Mgogoro wa kibinadamu Gaza unatisha
(last modified Mon, 12 May 2025 11:12:23 GMT )
May 12, 2025 11:12 UTC
  • Wamorocco: Mgogoro wa kibinadamu Gaza unatisha

Wananchi wa Morocco wameandamana kuunga mkono Wapalestina wanaoishi katika Ukanda wa Gaza, wakitangaza mshikamano wao na watoto wa eneo hilo la Palestina lililozingirwa ambao wanakabiliwa na njaa, kiu na maradhi; huku mgogoro mbaya wa kibinadamu uliosababishwa na Wazayuni ukiendelea kuwasakama.

Waunganji hao wa Palestina nchini Morocco waliingia katika mitaa ya Tangier Jumapili usiku, wakielezea mshikamano wao na watoto wa Gaza ambao wanakabiliwa na njaa na kutonana na vita na vizingiti vinavyowekea eneo hilo.

Huku wakinyanyua juu tochi za simu za simu zao za rununu, waandamanaji hao wametangaz akusikitishwa na njaa inayoendelea kuwakabili Wapalestina, kuendelea kuzingirwa Gaza, na mgogoro kibinadamu unaowakabili Wapalestina wa eneo hilo, hasa watoto.

Washiriki wa maandamano hayo pia wamesisitiza uungaji mkono wao kwa malengo matukufu ya Wapalestina na kupinga kuanzishwa uhusiano wa kawaida na utawala wa Kizayuni wa Israel. Makubaliano ya kuweko uhusiano wa kawaida kati ya Morocco na utawala wa Kizayuni yalifikiwa mwezi Disemba 2020. 

Tangu kutiwa saini mkataba huo, wananchi wa Morocco ambao wamejikita kwenye kuliunga mkono taifa la Palestina, wameonesha mara kwa mara upinzani wao dhidi ya maamuzi ya watawala wa nchi hiyo kupitia kufanya maandamano mikubwa huko Rabat na kwenye miji mingine.

Maandamano ya jana usiku ya kutangaza  mshikamano na Wapalestina, yaliwashirikisha pia watoto wa Morocco ambao walibainisha huruma na mshikamano wao kwa wenzao huko Gaza.