Rais Pezeshkian: Nchi za eneo zinaweza kutatua matatizo yao bila kusimamiwa
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i136640-rais_pezeshkian_nchi_za_eneo_zinaweza_kutatua_matatizo_yao_bila_kusimamiwa
Rais Masoud Pezeshkian wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza kwamba kuanzisha amani na utulivu ndiyo "njia ya maisha kwa sayari hii ndogo," akisisitiza kuwa nchi za eneo zinaweza kutatua matatizo yao bila kusimamiwa na kwamba, hakuna nchi itakayofaidika na vita, migogoro, vurugu, na umwagaji damu.
(last modified 2026-02-15T03:27:25+00:00 )
Feb 15, 2026 03:27 UTC
  • Rais Pezeshkian: Nchi za eneo zinaweza kutatua matatizo yao bila kusimamiwa

Rais Masoud Pezeshkian wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza kwamba kuanzisha amani na utulivu ndiyo "njia ya maisha kwa sayari hii ndogo," akisisitiza kuwa nchi za eneo zinaweza kutatua matatizo yao bila kusimamiwa na kwamba, hakuna nchi itakayofaidika na vita, migogoro, vurugu, na umwagaji damu.

Rais Pezeshkian amesema hayo katika hotuba yake kwenye Kongamano la Kimataifa la "Korido ya Iran 2026" kuhusu fursa za uwekezaji na ufadhili wa njia za usafiri wa reli na barabara, Rais Pezeshkian amesisitiza kwamba, ikiwa kuna vikwazo au matatizo yanayozuia ushirikiano katika maeneo yanayoshughulikiwa na mkutano huo, Iran iko tayari kuyashughulikia ndani ya mifumo ya kisayansi na utaalamu wa kiufundi kulingana na uzoefu uliofanikiwa.

Pezeshkian alizungumzia uhusiano wa kikanda, akisema: "Tunazichukulia nchi jirani kama ndugu, marafiki, na hata watu wetu wenyewe," akisisitiza kuwepo kwa uhusiano wa kihistoria, kikabila, na kitamaduni unaoendelea kwa maelfu ya miaka na Azerbaijan, Iraq, Kurdistan, Uturuki, Afghanistan, Pakistan, na Turkmenistan, na kuongeza kwamba mipaka ya mataifa haya haijakata uhusiano huu.

Rais wa Iran amesisitiza haja ya kuanzisha amani na utulivu, akisema kwamba njia hii ndiyo "njia ya maisha kwa sayari hii ndogo," akisisitiza kwamba, hakuna nchi itakayopata chochote kutokana na vita, migogoro, vurugu na umwagaji damu, na kutoa wito wa kuundwa kwa mazingira ambayo yanahakikisha kuishi kwa amani, usalama na utulivu kwa vizazi vya sasa na vijavyo.

Aidha amesema: "Kufungua upya njia za kikanda kutaendeleza amani, maendeleo, sayansi na uwezeshaji wa pande zote. Nchi zinaweza kuimarishana kwa kubadilishana utaalamu katika sekta za kiuchumi, viwanda, matibabu, utamaduni na kilimo. Muunganisho mkubwa utaboresha usalama na ukuaji wa uchumi kwa pande zote zinazohusika."