Dec 09, 2023 15:04 UTC
  • Iran: Operesheni ya Kimbunga cha al Aqsa imeisambaratisha Israel

Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza kuwa, operesheni ya Kimbunga cha al Aqsa imeusambaratisha vibaya utawala wa Kizayuni wa Israel.

Hossein Amir-Abdollahian amesema hayo leo (Jumamosi) katika kikao maalumu kwa mnasaba wa Siku ya Mwanafunzi kwenye Chuo Kikuu cha Tehran na kuongeza kuwa, mashirika saba ya kijasusi ya Israel yalikuwa yanafanya kazi usiku na mchana kuchunguza harakati za Wapalestina, lakini pamoja na hayo, HAMAS imeendesha operesheni ya kishujaa ya  #Kimbunga_cha_al- Aqsa na kuwaweka mdomo wazi watu wote.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran ameongeza kuwa, leo hii uamuzi wa makundi ya muqawama ni kuzishambulia pia kambi za kijeshi za Marekani za eneo hili kwani Washington ndiye muungaji mkono mkuu wa jinai za utawala wa Kizayuni.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran akihutumia wanachuo katika Chuo Kikuu cha Tehran

 

Amesema, Wamarekani wametutumia ujumbe hapa Iran na kuitaka iyazuie makundi ya muqawama yasiendeleze mashambulizi yao kwenye kambi za kijeshi za Marekani katika eneo hili, lakini sisi tumewaambia Wamarekani kwamba makundi hayo yako huru na yanachukua maamuzi yao kwa uhuru kamili.

Sisi tunaheshimu maamuzi yao ya kuendelea kuliunga mkono taifa la Palestina. Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran ameongeza kuwa, Marekani na Israel hazina stratijia maalumu ya kuendeleza vita na namna ya kuvisimamisha.

Amma kuhusu Afghanistan, Amir-Abdollahian amesema, ushauri wa Iran ni kuundwa serikali kubwa itakayoshirikisha pande zote huko Afghanistan na inaendeleza juhudi zake za kidiplomasia kuhusu suala hilo.

Amesema, kundi la Taliban si kundi la Daesh (ISIS) bali kundi hilo ni uhakika unaotawala Afghanistan hivi sasa na kuongeza kuwa, baadhi ya wanachama wa kundi la Taliban wanapambana na kupigana vita na Daeshi hivi sasa, hivyo nchi jirani zina wajibu wa kufanya juhudi za kulisaidia taifa la Afghanistan kupata usalama na utulivu zaidi.

Tags