Israel iliidondoshea Gaza mabomu 22,000 ya US ndani ya wiki 6
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i105926-israel_iliidondoshea_gaza_mabomu_22_000_ya_us_ndani_ya_wiki_6
Ripoti mpya imefichua kuwa, utawala haramu wa Israel ulidondosha zaidi ya mabomu 22,000 uliopewa na Marekani katika Ukanda wa Gaza, katika kipindi cha wiki sita za kwanza za mashambulizi ya kinyama dhidi ya Wapalestina wa ukanda huo.
(last modified 2023-12-12T23:17:05+00:00 )
Dec 12, 2023 23:17 UTC
  • Israel iliidondoshea Gaza mabomu 22,000 ya US ndani ya wiki 6

Ripoti mpya imefichua kuwa, utawala haramu wa Israel ulidondosha zaidi ya mabomu 22,000 uliopewa na Marekani katika Ukanda wa Gaza, katika kipindi cha wiki sita za kwanza za mashambulizi ya kinyama dhidi ya Wapalestina wa ukanda huo.

Gazeti la Washington Post huku likinukuu taarifa za kijasusi zilizokabidhiwa Kongresi ya Marekani limeripoti kuwa, Israel ilitumia mabomu hayo ya kuelekezwa na yasiyo ya kuelekezwa ya Marekani ndani ya wiki sita katika Ukanda wa Gaza, moja ya maeneo yenye msongamano mkubwa wa watu duniani.

Ripoti hiyo imeeleza kuwa, silaha zilizoundwa na Marekani zimekuwa na nafasi kubwa katika hujuma na mashambulzi ya kutisha ya Israel dhidi ya wakazi wa Ukanda wa Gaza.

Kwa mujibu wa ripoti ya gazeti la Washington Post, kwa wastani Israel ilidondosha bomu moja lililotengezewa Marekani kwa kila Wapalestina 100 wa Ukanda wa Gaza katika muda huo uliotajwa.

Mabomu ya US yanavyoua na kuharibu miundimbinu ya Gaza

Kabla ya hapo, Ofisi ya Habari ya Ukanda wa Gaza ilisema kuwa, jeshi katili na vamizi la Israel limedondosha makumi ya maelfu ya tani za mada za milipuko katika Ukanda wa Gaza, na kwamba tani hizo ni sawa na bomu la nyuklia lililotumika huko Hiroshima nchini Japan.

Israel ilianzisha vita vyake vya umwagaji damu kwenye Ukanda wa Gaza Oktoba 7 baada ya mashambulizi ya kushtukiza, yaliyopewa jina la Kimbunga cha al-Aqsa ya wanamuqwama wa Hamas.

Tangu kuanza vita hivyo utawala wa Israel umekuwa ukifanya jinai za kivita huko Gaza na kuwaua zaidi ya Wapalestina 18,400, wengi wao wakiwa ni wanawake na watoto.