Kaani: Ugaidi ni hatari iliyoenea kwa serikali na mataifa yote
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i106970-kaani_ugaidi_ni_hatari_iliyoenea_kwa_serikali_na_mataifa_yote
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza kuwa ugaidi ni hatari kubwa kwa serikali na mataifa yote na kwa amani na usalama wa dunia. Nasser Kanani ameeleza haya katika radiamali yake kwa shambulio la kigaidi lililotekelezwa katika maziara ya mashahidi wa mji wa Kerman huko kusini mashariki mwa Iran.
(last modified 2024-01-08T08:57:25+00:00 )
Jan 08, 2024 08:57 UTC
  • Kaani: Ugaidi ni hatari iliyoenea kwa serikali na mataifa yote

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza kuwa ugaidi ni hatari kubwa kwa serikali na mataifa yote na kwa amani na usalama wa dunia. Nasser Kanani ameeleza haya katika radiamali yake kwa shambulio la kigaidi lililotekelezwa katika maziara ya mashahidi wa mji wa Kerman huko kusini mashariki mwa Iran.

Tarehe 4 mwezi huu wa Januari magaidi katili walitekeleza miripuko ya kigaidi katika mkusanyo wa watu waliokuwa wakielekea kwenye makaburi ya mashahidi wa mji wa Kerman na kuwaua shahidi wanawake, wanaume na hata watoto wadogo. Hujuma hiyo ya kigaidi ilitekelezwa sambamba na marasimu ya kumbukumbu ya mwaka wa nne tangu kuuliwa shahidi Luteni Jenerali Qassim Suleimani aliyekuwa Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC). 

Shambulio la kigaidi katika mji wa Kerman 

Nasser Kanani Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran leo Jumatatu amezungumza na waandishi wa habari hapa Tehran katika mkutano wake wa kila wiki na akasema kuhusu hujuma ya kigaidi ya huko Kerman kwamba: Wale wanaotumia ugaidi kusogeza mbele malengo yao maovu watambue kuwa wajibu wa kisheria, kimataifa, kibinadamu na kimaadili unatokana na kuungwa kwao mkono makundi ya kigaidi na ni lazima wawajibike. 

Shirika la habari la Farsi limeripoti kuwa, Kanani ameongeza kuwa, katika mazungumzo na pande za Magharibi, siku zote tumekuwa tukieleza kuwa hakuna ugaidi mzuri au mbaya na kwamba tishio hilo limeenea kote duniani na linatishia usalama, amani na usalama wa mwanadamu. 

Kanani amesema Daesh kundi la kigaidi lililoasisiwa na mashirika ya ujasusi na intelijensia ambayo si ya kikanda ambayo wakati fulani yalitangaza na kukiri kuhusika kwayo moja kwa moja katika kusababisha hali hii, katika miaka kadhaa iliyopita.

ISIS, kama kundi lililoundwa na idara za ujasusi na usalama zisizo za kikanda, ambalo wakati mwingine lilitangaza na kukiri kuhusika kwake moja kwa moja katika kusababisha hali hii limetekeleza matukio mbalimbali ya kigaidi katika eneo; na katika miaka kadhaa ya karibuni kundi hilo limetekeleza hujuma hatari za kigaidi katika eneo hili na nje ya eneo ambapo nchi nyingi za magharibi mwa Asia zimekuwa wahanga wa ugaidi wake. 

Katika sehemu nyingine ya mkutano na waandishi wa habari, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran ameashiria matukio ya Gaza na kusema: Serikali za Magharibi na Ulaya nyuma ya nara wanazopiga zinapaswa kuchukua hatua za kivitendo na kusitisha uungaji mkono wao wa kilojistiki, kijeshi na kiusalama kwa utawala wa Kizayuni na badala yake ziushinikize pakubwa utawala huo ili usimamishe vita vyake vya kidhulma dhidi ya wakazi wa Ukanda wa Gaza.  

Kanani amesema Iran inaunga mkono ubunifu na mazungumzo yoyote ya Palestina kwa lengo la kuimarisha umoja na mshikamano.