Kubainishwa misimamo ya Iran kuhusu haki za binadamu katika Mkutano wa Geneva
Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amewasilisha misimamo na mitazamo ya Iran kuhusu haki za binadamu katika mkutano wa 55 wa Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa mjini Geneva Uswisi.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Hossein Amir-Abdollahian Jumatatu ya jana (Februari 26) aliwasili Geneva, Uswisi kwa ajili ya kushiriki katika mkutano wa 55 wa Baraza la Haki za Kibinadamu la Umoja wa Mataifa.
Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Iran amehutubia katika kikao cha ngazi ya juu cha mkutano wa kila mwaka wa Baraza la Haki za Binadamu na sehemu ya ngazi ya juu ya Kongamano la Upokonyaji Silaha la Umoja wa Mataifa. Sambamba na kushiriki katika kikao kidogo cha Palestina, Amir Abdollahian ameeleza misimamo na mitazamo ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kuhusu Palestina na mgogoro unaoendelea Gazah na Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan huko Palestina.
Katika miaka ya hivi karibuni, Marekani na serikali za Ulaya zimejaribu kujionyesha kama wafuasi wa haki za binadamu na zimetumia vyombo vya habari mashuhuri na vyenye mitazamo sawa na ya kwao ili kuonyesha sura ya kibinadamu.
Serikali za Magharibi, daima zimekkuwa zikilitumia suala la haki za binadamu kama wenzo wa malengo ya kisiasa na huzitambuliisha nchi huru ambazo haziko tayari kuburuzwa nazo kuwa ni maadui wa haki za binadamu. Matukio ya kisiasa ya ulimwengu katika miaka ya hivi karibuni yamefichua kwamba, haki za binadamu zinazopigiwa upatu na serikali za Magharibi zina vigezo vyake.
Serikali za Magharibi zimenyamazia kimya mara chungu nzima mauaji makubwa ya halaiki hususan ya Waislamu katika sehemu mbalimbali za dunia, na hazikuwa tayari kulipa hata gharama ndogo kabisa ya suala hili.
Mauaji ya kimbari ya Waislamu wa Bosnia na Herzegovina na Myanmar ni miongoni mwa kesi ambazo wadai wa haki za binadamu wamenyamazia kimya na kuwa pamoja na watendaji wa jinai hizo na kuunga mkono vitendo vyao.
Mfano mwingine wa wazi ni ubaguzi na muamala na Waislamu katika nchi nyingi za Ulaya na Magharibi, ambapo serikali za Magharibi hata zinaweka mipaka ya ibada na mavazi ya Waislamu kwa kuweka sheria za upande mmoja.
Uungaji mkono wa viongozi wa nchi za Ulaya kwa vitendo vya kikatili vya makundi ya kibaguzi pamoja na mashambulizi ya nyama na mauaji ya Waislamu katika nchi hizi, ni mifano mingine ya ada hizi za kujikariri na za kibaguzi katika nchi za Magharibi.
Lakini jambo la kuzingatia katika kutoa tathmini na uchambuzi wa kwa nini sera na vitendo vya kibaguzi vya serikali za Magharibi ni ukimya wao kuhusiana na matusi na kuvunjiwa heshima Qur'ani Tukufu na thamani za Kiislamu, na kwamba katika sheria za nchi hizo hakuna sheria hata ya kuwashtaki na kuwaadhibu watu waovunjia heshima matukufu ya wengine.
Mkabala wake, ni uungaji mkono wa kibubusa wa Marekani na madola ya Magharibi kwa fikra za Kizayuni, kiasi kwamba maswali na kutilia shaka kwa namna yoyote kuhusiana na ngano ya holocaust yaani mauaji ya halaiki dhidi ya Wayahudi yanayodaiwa kufanywa na utawala wa Kinazi wa Ujerumani chini ya uongozi wa Adolf Hitler katika Vita vya Pili vya Dunia ni hatua ambayo hukabiliwa na adhabu kali ya faini na kifungo.
Kuwepo Amir-Abdollahian mjini Geneva na kuwasilisha misimamo ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran bila shakka ni tukio muhimu na lenye taathira kubwa, kwa sababu mitazamo tofauti kuhusu haki za binadamu ni muhimu kwa watu huru na umma kwa ujumla katika dunia ya leo, kinyume na madai na misimamo ya serikali za Magharibi.
Kuzungumziwa masuala kama vile kuheshimu dini za Mwenyezi Mungu na thamani za kimaanawi katika jamii tofauti, na kueleza thamani za Kiislamu kuwa ni kanuni thabiti na ya kudumu kwa Iran ni miongoni mwa masuala ambayo Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Iran atayajadili katika Mkutano wa Geneva na kubainisha umuhimu wa hilo baina ya nchi za Kiislamu kwa ulimwengu wa Magharibi.
Suala jengine la msingi katika mkutano huu wa kilele ni kurejeshwa haki zilizonyakuliwa za Palestina na uungaji mkono wa daima wa Iran kwa haki za watu wa Palestina.
Tangu ilipotekelezwa operesheni ya kimbunga ya Al-Aqswa Oktoba mwaka jana (2023) na kuenea jinai na mauaji ya kimbari yaliyopangwa huko Gazah, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imefanya juhudi athirifu katika mikutano tofauti ya kimataifa na ya kieneo ili kuwafahamisha walimwengu .
Kwa kuzingatia kwamba, Iran ni nchi yenye ushawishi mkubwa na ina mitazamo mbalimbali kuhusu haki za binadamu, ni jambo liisilo na shaka yoyote kkwamba, pendekezo lake katika mkutano wa Geneva linaweza kufungua njia ya matatizo ya leo katika eneo na matukio ya kimataifa.