Mar 01, 2024 03:47 UTC
  • Uchaguzi nchini Iran unafanyika leo Ijumaa

Uchaguzi wa duru ya 12 ya Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu (Bunge) na Baraza la Wataalamu Wanaomchagua Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu unafanyika leo Ijumaa kote nchini ambapo wagombea watawania viti 290 vya Bunge na 88 vya Baraza la Wataalamu Wanaomchagua Kiongozi Mkuu wa nchi.

Kampeni za uchaguzi huo ambazo zilianza wiki moja iliyopita zilimazika asubuhi ya jana kwa mujibu wa kifungu cha Katiba ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. 

Zaidi ya wagombea 15,200 wanawania viti 290 vya ubunge, 30 kati ya hivyo ni vya mji mkuu, Tehran, ambao unatambuliwa kuwa jimbo kubwa zaidi la uchaguzi nchini.

Wapiga kura wa Iran, ambao idadi yao ni milioni 61, 172 elfu na 298, pia watachagua wajumbe wa Baraza la Wataalamu wa Uongozi, linalojumuisha wanachama 88 wanaohudumu kwa kipindi cha miaka 8. Watu 144 wamepasishwa kuwania nafasi hizo. 

Taarifa iliyotolewa na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Iran inaonesha kuwa, idadi ya watu waliojiandikisha kugombea viti vya Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu ya Iran (Bunge) imevunja rekodi ya ile iyosajiliwa tangu baada ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu, mwaka 1979.

Taarifa hiyo inasema, wagombea 15,200 wameidhinishwa na vyombo husika kuwania viti 290 vya Bunge, idadi ambayo inaweka rekodi mpya tangu baada ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu mwaka 1979.

Orodha ya wagombea waliotimiza masharti inajumuisha majina ya wanawake 1,713, ambayo ni zaidi ya mara mbili ya 819 waliogombe viti vya Bunge hapa nchini mwaka 2020. 

Tags