Mar 04, 2024 13:14 UTC
  • Iran yamnyonga gaidi aliyekuwa akihudumia shirika la  kijasusi la Israel, Mossad

Iran imemnyonga gaidi wa aliyekuwa akitumikia shirika la kijasusi la utawala haramu wa Israel, Mossad ambaye alipanga kutega bomu katika karakana ya Wizara ya Ulinzi huko Isfahan, katikati mwa Iran.

Januari 28, 2023, Wizara ya Ulinzi ya Iran ilichapisha taarifa kwamba kkulikuwa shambulio lililofeli la kushambulia karakana ya wizara huyo kwa kutumia ndege ndogo zisizo na rubani. Kufuatia operesheni ya kikosi cha ulinzi wa anga, mmoja ya ndege hizo ndogo ilitunguliwa na zingine mbili zilinaswa

Kwa mujibu wa Taarifa ya Kanali ya Sahab, Hujjatul Islam Esdaleh Jafari, mkuu wa Idara ya Mahakama ya mkoa wa Isfahan, amesema baada ya shambulio lililofeli kwenye karakana ya Wizara ya Ulinzi huko Isfahan, gaidi aliyekuwa ametumwa na Mossad alitoroka Iran kwa utambulisho bandia, lakini 13 baadaye, kwa jitihada za mahakama na vikosi vya usalama vya Iran alikamatwa katika moja ya nchi jirani.

Kulingana na Mkuu wa Idara ya Mahakama katika jimbo la Isfahan, hukumu ya kifo ya gaidi huyo wa Mossad imetekelezwa jana Machi 3, 2024.

Mwezi Januari pia Idara ya Mahakama ya Iran iliwanyonga watu wanne waliopatikana na hatia ya kufanya kazi na shirika la ujasusi la utawala haramu wa Israel, Mossad, na kupanga njama ya shambulio la bomu dhidi ya kiwanda cha Wizara ya Ulinzi katika mkoa wa Isfahan katikati mwa Iran.

Shirika la habari la Mizan, lenye uhusiano na Idara ya Mahakama ya Iran, limesema magaidi hao wanne, waliotambuliwa kwa majina ya Mohammad Faramarzi, Mohsen Mazloum, Vafa Azarbar na Pejman Fatehi, waliingia Iran kinyume cha sheria kutoka eneo lenye mamlaka ya ndani la Kurdistan nchini Iraq.

Taarifa hiyo imesema, mnamo Julai 23, 2022, walikuwa wakipanga kutekeleza operesheni ya kulipua jengo la karakakana katika mji wa Najafabad, mkoani Isfahan ambacho huunda zana za kijeshi na vipuri vya makombora kwa ajili ya Wizara ya Ulinzi.

Mnamo tarehe 29 Disemba mwaka jana pia magaidi waliokuwa wakishirikiana na Mossad walinyongwa katika mkoa wa kaskazini magharibi mwa Iran wa Azarbaijan Magharibi baada ya kukutwa na hatia ya kupanga njama dhidi ya usalama wa nchi.

Mwezi Februari mwaka huu pia Wizara ya Intelijensia ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imetangaza kuwa imefichua vibaraka kadhaa wa shirika la ujasusi la Israel, Mossad katika nchi 28 duniani.

Tags