Apr 28, 2024 07:20 UTC
  • Kan'ani: Iran ni katika washirika muhimu wa amani duniani

Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Jamhuri ya Kiislamuu ya Iran amesema, Iran imegeuza vikwazo kuwa fursa ya kuimarisha na kuendeleza uwezo wake wa kiulinzi na kijeshi, na ni miongoni mwa washirika muhimu wa jami ya kimataifa katika kuhakikisha amani na usalama wa kieneo na kimataifa na kupambana na ugaidi wa kimataifa.

Nasser Kan'ani, amelaani vikali hatua ya Marekani, Uingereza na Canada ya kuwawekea marufuku baadhi ya watu katika jeshi la Iran kama ambavyo amelaani pia uamuzi wa Bunge la Ulaya na kuibua tuhuma dhidi ya Iran na kuzikosoa nchi chache za Ulaya kutokana na kuendelea na mbinu kandamizi ya utawala wa Marekani.

Kanaani ameongeza kuwa: Uwezo wa kijeshi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran unalingana na mahitaji yake katika kuhakikisha usalama na maslahi ya taifa, kulinda mamlaka na umoja wa ardhi, na ulinzi halali na uzuiaji vitisho na uchokozi wowote wa nje Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na kwamba, taifa hili linahesabiwa kuwa mmoja wa washirika muhimu wa jamii ya kimataifa katika kuhakikisha amani na usalama wa kikanda na kimataifa na kupambana na ugaidi wa kimataifa.

Aidha amesema, kutumia wenzo wa vikwazo dhidi ya uwezo wa kiulinzi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran hakuwezi kutia kasoro katika irada ya serikali na wananchi wa Iran ya kuimarisha nguvu ya taifa kwa lengo la ulinzi halali na madhubuti wa mamlaka ya kujitawala ya Iran, umoja wa ardhi, usalama na maslahi ya taifa na badala yake, kinyume na matakwa ya nchi zilizoweka vikwazo, nchi yetu imegeuza vikwazo hivi kuwa fursa ya kujitegemea na kujitosheleza katika kuimarisha na kuendeleza uwezo wetu wa ulinzi na kijeshi.