Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu atembelea Maonyesho ya Vitabu ya Tehran
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i111724-kiongozi_muadhamu_wa_mapinduzi_ya_kiislamu_atembelea_maonyesho_ya_vitabu_ya_tehran
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ametembelea Maonyesho ya Kimataifa ya Vitabu mjini Tehran
(last modified 2024-05-13T08:34:25+00:00 )
May 13, 2024 08:34 UTC
  • Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu atembelea Maonyesho ya Vitabu ya Tehran

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ametembelea Maonyesho ya Kimataifa ya Vitabu mjini Tehran

Kwa mujibu wa idara ya habari ya  Ofisi ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ametembelea Maonyesho ya 35 ya Kimataifa ya Vitabu leo ​​(Jumatatu) ambayo yanafanyika katika Eneo la Muswala wa Imam Khomeini (RA).

Akiwa katika maonyesho, Kiongozi Muadhamu amezungumza na wachapishaji, waandishi na wamiliki wa maduka ya vitabu, na kufahamishwa kwa karibu kuhusu habari za uchapishaji na hali ya soko la vitabu, pamoja na kiwango cha kukubalika maonyesho hayo.

Maonyesho hayo yalizinduliwa Jumatano, yakikaribisha zaidi ya wachapishaji 2,500 wa Iran na 60 wa kigeni ambao wamewasilisha vitabu vyao vipya zaidi katika hafla hiyo.

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu akiwa katika Maonesho ya Kimataifa ya Vitabu ya Tehran

Yakiendeshwa chini ya kauli mbiu "Tusome na Tuunde," Maonyesho ya 35 ya Kimataifa ya Vitabu ya Tehran yataendelea hadi Mei 18.

Yemen imepewa hadhi ya mgeni maalum katika maonyesho hayo ya vitabu mwaka huu kwa lengo la kuimarisha utamaduni wa muqawama au mapambano ya Kiislamu.