Leo ni kumbukumbu ya miaka 35 tangu kuaga dunia Imam Khomeini
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i112492-leo_ni_kumbukumbu_ya_miaka_35_tangu_kuaga_dunia_imam_khomeini
Wananchi wa Iran leo wanafanya kumbukumbu ya miaka 35 tangu kuaga dunia Imam Ruhullah Khomeini, muasisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
(last modified 2026-02-05T09:20:29+00:00 )
Jun 02, 2024 23:57 UTC
  • Leo ni kumbukumbu ya miaka 35 tangu kuaga dunia Imam Khomeini

Wananchi wa Iran leo wanafanya kumbukumbu ya miaka 35 tangu kuaga dunia Imam Ruhullah Khomeini, muasisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Imam Khomeini aliongoza mapinduzi ya wananchi dhidi ya utawala dhalimu wa Shah ambayo yalipata ushindi mwaka 1979.

Kumbukumbu hiyo inafanyika leo kkatika Haram ya Imam Khomeini na Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Khamenei anatarajiwa kuhutubia umma kwa mnasaba huo kutoka katika Haram hiiyo.

Mapinduzi yaliyoongozwa na Imam Khomeini yalipelekea kuhitimishwa utawala wa mfalme Shah na kuasisiwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Siku kama ya leo miaka 35 iliyopita mwaka 1989, Imam Ruhullah Musawi Khomeini (M.A) mwasisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran aliaga dunia akiwa na umri wa miaka 86. Ulimwengu wa Kiislamu uligubikwa na majonzi na huzuni kubwa kutokana na kutangazwa kifo cha Imam.

Wananchi wa Iran miaka 35 iliyopita wakati walipokuwa wakiusindikiza na kuuaga mwili wa Imam Khomeini

 

Imam Khomeini (M.A) alizaliwa tarehe 24 Septemba 1902 katika mji wa Khomein ulioko katikati mwa Iran. Alianza kujishughulisha na siasa sambamba na masuala ya kielimu na kiutamaduni. Mapambano ya Imam dhidi ya utawala wa Shah na uingiliaji wa Marekani nchini Iran yalishtadi mwaka 1963 na kupelekea Imam Khomeini kupelekwa uhamishoni. Imam alibobea katika taaluma mbalimbali, na mbali na kuwasomesha wanafunzi wengi na kutoa hotuba nyingi za kihistoria, alikuwa pia mwandishi hodari wa vitabu.